Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kagasheki (wa pili kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr. Mary Nagu (kulia), Mkuu wa Mko a wa Tabora, Fatuma Mwasa (watatu kushoto ), Mbunge wa Tabora Mjini Aden Rage (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Nyuki Tabora, Liana Hassan (watatu kulia) wakiimba wimbo wa Taifa katika mahafali ya Chuo cha Nyuki cha Tabora ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu Agosti 30, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaaga wahitimu wa Chuo cha Nyuki cha Tabora baada ya kuwatunuku vyeti, Diploma katika mahafali ya Chuo hicho jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mizinga ya kisasa katika maonyesho ya Chuo cha Nyuki cha Tabora akiwa mgeni katika mahafali ya Chuo hicho mjiniTabora Agosti 30, 2013. Wapili kushoto ni mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Chuo hicho, Liana Hassan.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama baadhi ya vifaa vya kusindika asali katika maonyesho ya Chuo cha Nyuki cha Tabora ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo hicho. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Ukwekezaji, Dr. Mary Nagu na Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Chuo hicho, Liana Hassan.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama baadhi ya vifaa vya kusindika asali katika maonyesho ya Chuo cha Nyuki cha Tabora ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo hicho. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Ukwekezaji, Dr. Mary Nagu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua bwalo la chakula la Chuo cha Nyuki cha Tabora akiwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Chuo hicho jana. Wapili kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Hamisi Kagasheki na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Liana hassan na Watatu Kulia ni Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage.