Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amethibitisha hayo jioni hii Bungeni mjini Dodoma.
Mawaziri hao waliotenguliwa nyadhifa zao ni: Mhe. David Mathayo David wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki wa Maliasili na Utalii, Mhe. Emmanuel Nchimbi wa Mambo ya Ndani na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha wa Ulinzi.
Mhe. Kagasheki alitangaza kujiuzulu mapema kabla uamuzi huo uliotangazwa na Waziri Mkuu.
********************
Hizi ni baadhi ya post kwenye wall ya Facebook ya Mh Zitto Kabwe kufuatia kusomwa kwa Taarifa ya Kamati ya BUNGE kuhusu Operesheni Tokomeza.