Kwa mara nyingine kwa wale wapenzi wa Nyama Choma yaani “ Nyama Choma Festival “ ule wakati adhimu wa kujilamba vidole umewadia namaanisha Jumamosi hii katika viwanja vya Posta jijini Dar-Es-Salaam.
Akizungumza na waandishi mwaandaaji wa tamasha hilo Carol Ndosi alisema kama ilivyo ada macho yote yataelekezwa pale viwanja vya posta.” Katika edition hii kuna maboresho kadhaa ambayo yamefanyika, kwanza tumeongeza mabanda yatakayokuwa yanatoa huduma ya nyama pamoja na vinywaji.
Kwa ujumla tunategemea kuwa na zaidi ya 20 stalls (vibanda) kwa ajili ya nyamana vinywaji vya aina mbali mbali ambapo mtu atakuwa na different choices za nyama na vinywaji . Baadhi ya hizo ni pamoja na Kennys, Bits n Crumbs, The grille, Dodoma Wine, stall, Shomas, Rose Garden, Blind Tiger stall, Detahs, Carols kitchen, Heineken Lounge, Aminas, Iranian Grill, Nigerian Nyama, Tikka Grill, Mbudya restaurant, belinda resort, fyatanga, saucy q hut and Spurs.
Tunategemea kuwa na michezo mbali mbali ikiwemo kwa ajili ya watoto Jumping Castles, Foosball, Pool Table na pia tunategemea kuonyesha live mechi za ligi ya Uingereza yaani Premier League kwa wale ambao ni wapenzi wa mchezo huo”. Alisema Carol.