Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela anasemekana kuwa hali yake inaendelea vizuri baada ya kulazwa hospitali kwa muda wa siku tisa sasa.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa Mandela ameendelea kuwa pamoja na familia yake katika hospitali ya mjini Pretoria ambako anapatiwa matibabu.
Katika hotuba, Zuma pia ametoa wito kwa watu kujiunga naye ili kumtakia Mandela siku njema ya maadhimisho ya siku ya kinababa duniani
Mandela mwenye umri wa miaka 94, anasumbuliwa na maambukizi katika mapafu, ikiwa ni mara ya nne kulazwa hospitalini kwa ajili ya matibabu tangu Desemba mwaka jana.