Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Wakazi wa Manyoni- Singida watakiwa kuuza asali au kuku mmoja ili kupata 5,000 ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii-CHF.

$
0
0

E83A0437

Mkuu wa wilaya ya Manyoni  Fatma H.Toufiq, akizungumza kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wananachi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) uliofanyika katika kijiji cha Itagata jimbo la Manyoni magharibi .Manyoni ni wilaya ya mwisho kati ya wilaya sita za mkoa swa Singida kwa wananchi wake kujiunga na mfuko huo.

E83A0419

Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni Dk.Rahim Hangai akitoa taarifa yake juu ya mfuko wa afya ya jamii kwenye uzinduzi wa mfuko huo uliofanyika katika kijiji cha Itagata tarafa ya Itigi.

E83A0432

Afisa wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Singida Isaya Sheikifu, akitoa taarifa yake juu ya uzinduzi wa umahasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii uliofanyika katika kijiji cha Itagata wilaya ya Manyoni.

E83A0409

Afisa wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)  mkoa wa Singida Agnes Chami akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Manyoni,Fatma H.Toufiq, msaada wa shuka uliotolewa na NHIF kwa naadhi ya zahanati za wilaya ya Manyoni.

E83A0416

Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii uliofanyika kiwilaya katika kijiji cha Itagata.(Picha na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu.

Kaya  4,133 kati ya kaya 58,326 za halmashauri ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida, ndizo zilizojiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), kitendo kinachochangia utoaji wa huduma ya afya ushindwe kukidhi mahitaji ya wananchi.

Idadi hiyo ya Kaya zilizojiunga na CHF ni sawa na asilimia 19 tu ya Kaya zote 58,326 za halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.

Hayo yamesemwa juzi na mganga

Mganga Mkuu wa wilaya ya Manyoni Dkt. Rahim Hangai ametoa takwimu hizo muda mfupi kabla hajamkaribisha Mkuu wa Wilaya hiyo Fatma Toufiq, kuzindua zoezi maalum la uhamasishaji wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii ili wawe na uhakika zaidi ya kupata matibabu.

Kwa mujibu wa Dkt. Hangai, kaya yenye mume, mke mmoja na watoto wanne waliona umri wa miaka chini ya 18,wakilipa ada  ya shilingi 5,000 tu kujiunga na mfuko huo, watapata matibabu bila kuongeza fedha zo zote kwa kipindi cha mwaka mzima.

Akifafanua zaidi kuhusu wananchi kusua sua kujiunga na CHF, amesema hali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na kutokutolewa kwa elimu juu ya mfuko huo na faida zake.

Aidha,Dkt. Hangai  amesema katika kipindi cha kati ya Julai mwaka jana na Mei mwaka huu, zaidi ya shilingi 7.5 zimekusanywa ikiwa ni ada za wanachama na zaidi ya shilingi 8.8 za mallipo ya papo hapo.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha Itagata, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bi. Fatma Toufiq, amesema kwa vile wilaya ya Manyoni ni ya mwisho mkoani Singida kwa wananchi kujiunga na CHF, sasa ni lazima kukimbia ili kuhakikisha kaya nyingi zinajiunga na mfuko huo mapema iwezekanayo.

Toufiq amesema kwa vile CHF ina faida  nyingi, ikiwa ni pamoja na kumwezesha mwananchi kupata matibabu wakati wo wote pale anapokuwa mgonjwa bila hata kuwa amejiandaa kifaedha kwa matibabu.

Amesema kutokana na hali hiyo, inahitajika nguvu za ziada za kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo, ili kujihakikishia kupata matibabu wakati wote wanapopata maradhi.

Aidha amewataka wananchi kutumia mapato yatokanayo na asali wanayouza kwa sasa, kutumia shilingi 5,000 tu kutoka kwenye mauzo hayo, ili kujiunga na CHF au kuuza kuku moja.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles