Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all 1758 articles
Browse latest View live

Wananchi wenye hasira nchini Bolivia wamzika mtuhumiwa wa ubakaji na mauaji akiwa hai kwa kumtumbukiza katika kaburi la mtu aliyemuua.

$
0
0

A suspected rapist and murderer has been buried alive in the grave of his alleged victim by enraged villagers, according to reports.Santos Ramos, 17, had been identified by Bolivian police as a possible culprit in the death of 35-year-old Leandra Arias Janco.More than 200 residents took the law into their own hands, reportedly seizing the teenager during the woman's funeral earlier this week and burying him alongside his victim.The villagers in Colquechaca, in the Potosi district of Bolivia's southern highlands, then blocked a road to prevent police and prosecutors from reaching the area, according to an official.A witness who would not be named said Ramos was tied up before being thrown into the open grave, which was then filled with earth.Lynchings sometimes occur in rural and poor parts of Bolivia in the absence of a heavy police presence.

Wananchi wenye hasira nchini Bolivia wamemzika mtuhumiwa wa ubakaji na mauaji akiwa hai kwa kumtumbukiza katika kaburi la mtu aliyemuua.

Mtuhumiwa huyo Santos Ramos mwenye umri wa miaka 17, alitambuliwa na polisi wa Bolivia kuwa anaweza kuwa ndiye alihusika na kifo cha Leandra Arias Janco aliyekuwa na miaka 35.

Zaidi ya watu 200 waliamua kuchukua sheria mikononi, ambapo inaripotiwa kuwa walimkamata kijana huyo wakati wa mazishi ya mwanamke huyo aliyebakwa na kuuawa na kumzika pamoja nae.

Wanakijiji cha Colquechaca katika wilaya ya Potosi katika miinuko ya kusini mwa Bolivia, waliweka vizuizi barabarani kuwazuia polisi na waendesha mashita wasiingie eneo lililokuwa likifanyika mazishi hayo.

Shuhuda wa tukio hilo amedai kuwa Ramos alifungwa kamba kwanza kasha akatumbukizwa katika kaburi lililokuwa na mwili wa mwanamke aliyedaiwa kumuua na kasha kulifukia kwa udongo.

Matukio ya mauaji wakati mwingine hutoa katika maeneo ya vijijini na maeneo masikini ya Bolivia ambako hakuna hakuna ulinzi mkali wa polisi.

 


Hii ndio tarehe nyingine ya show ya Miaka 13 ya JayDee kwa wale ambao walikuwa bado hawajapata taarifa rasmi.

Serikali ya Ujerumani yatoa punguzo la kodi kwa mashoga walio katika ndoa.

$
0
0

ARCHIV - Ein schwules Paar läuft am 08.08.2009 im Stadtteil St. Georg in Hamburg vor Beginn des Christopher Street Day über die Straße. In fden Niederlanden kommen in Schulbüchern künftig auch homosexuelle Eltern vor. Nicht jeder ist begeistert. Foto: Jens Ressing dpa/lno (zu dpa 0006 vom 10.08.2010) +++(c) dpa - Bildfunk+++

Mahakama ya Shirikisho la Ujerumani imesema kuwa sheria inayowapa punguzo la kodi watu walio katika ndoa ya mume na mke pekee yao ni kinyume cha katiba.

Mahakama hiyo iliyoko mjini Karlsruhe imesema kuwa watu walio katika ndoa ya jinsia moja pia wanapaswa kunufaika na punguzo hilo la kodi ambalo linatolewa kwa watu walio katika ndoa.

Kulingana na uamuzi huo, watu walio katika ndoa ya jinsia moja watanufaika na punguzo hilo na itahesabiwa kuanzia mwaka 2001 ambapo Ujerumani ilizitambua kisheria ndoa za jinsia moja.

Serikali ya Angela Merkel inayofuata sera za mrengo wa kulia kwa muda mrefu imekuwa ikipinga haki sawa kati ya ndoa kati ya mume na mke na zile za watu wa jinsia moja.

Nani Kumrithi Miss Tanzania Brigit Alfred Taji la Redd’s Miss Sinza?

$
0
0
Warembo 11 kati ya 12 wanaopanda jukwaani leo kuwania Taji lenye Sifa Kuu mbili ya Redd’s Miss Sinza 2013, lakini pia linaloshikiliwa na Redd’s Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred, leo katika Ukumbi wa Meeda Club uliopo Sinza Mori. Katika shindano hilo litakalosindikizwa na burudani kabambe kutoka kwa Bendi mahiri ya African Stars, ‘Twanga Pepeta’, viingilii vitakuwa ni Sh. 20,000/= kwa VIP na Sh. 10,000/= kwa viti vya kawaida. Shindano hili limedhaminiwa na Redds Original, Mtandao wa Sufianimafoto Blog, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group na Salut5.com.
Mshiriki mwenye No, 9-SARAHY PAUL (23)..
Mshiriki mwenye No 8-HAPPYNESS MAIRA (19)
Mshiriki mwenye No, 11-NICOLE MICHAEL (21)
Mshiriki mwenye No, 5-PRISCA ELEMENT (20)
Mshiriki mwenye No, 3-MAUA ABDUL (18)
Mshiriki mwenye No, 7- AGNES SIMON (22)
Mshiriki mwenye No, 1-CATRINA LAURENCE (19)
 Mshiriki mwenye No, 6-JACQUELINE ROBERT (20)
 Mshiriki mwenye No, 4-DORIS MWAIPOPO (19) 

Mshiriki mwenye No, 10-MARTHA JOSEPH (19)
 Mshiriki mwenye No, 2-NASRA HASSAN (18)
 
Mwalimu wa warembo hao, Mwajay Model, akionyesha uwezo wa kusebeneka, wakati akifungua rasmi shoo ya warembo hao ya kujitambulisha katika Promosheni maalum ya utambulisho wa shindano lao iliyoandaliwa na kinywaji cha Redd’s katika Baa ya Mary Land Mwenge jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni mshereheshaji wa hafla hiyo fupi….. 

Warembo hao wakipozi kusubiri utaratibu baada ya kuwasili eneo la tukio jana usiku.

Warembo wakimshangilia mwenzao wakati akipita mbele kwenda kujitambulisha, ”sasa sijui na leo jioni huyu ndiye atakayeshangiliwa kama hivi?”

Mwalimu wa warembo hao, Majay (kulia) akipozi na warembo wake.
IMG_1476
Hapa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao….ya maandalizi….

Rais Putin wa Russia atengana na mkewe baada ya ndoa iliyodumu kwa miaka 30.

$
0
0

a_560x375

Rais Vladimir Putin wa Russia ametengana mkewe Lyudmila Alexandrovna baada ya kuishi maisha ya ndoa kwa miaka takriban 30.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 30 na mkewe wametoa tangazo hilo katika televisheni ya taifa.

Mkewe Lyudmila mwenye umri wa miaka 55 ambaye alimuoa mwaka 1983 alikuwepo pembeni yake wakati rais akitanga kutengana kwao.

Akijibu maswali alipoulizwa iwapo kwa sasa wanaishi tofauti rais huyo alisema ‘ndio’ na kuongeza kuwa kazi zake zinahusiana na kuonekana kwa jamii kila mawa huku watu wengine wanapenda na wengine hawapendi.

Amesema muda mrefu wamekuwa hawaonani na kila mtu amekuwa akiishi maisha yake kutokana na ratiba ya kazi zake.

Rais huyo na mkewe wana mabinti wawili Maria na Yekaterina ambao wote wanamiaka zaidi ya 20.

Lydmila amewahi kuonekana mara chache sana katika kipindi chote ambacho mumewe amekuwa katika nafasi za juu za kisiasa nchini humo.

Mara ya mwisho kuonekana pamoja hadharani ni wakati wa sherehe za kumuapisha Putting kuiongoza nchi hiyo kwa awamu ya tatu Mei 7 mwaka jana.

Wanandoa hao walioana Julai 28 mwaka 1983 wakati Putin akiwa afisa kijana katika shirika la kijasusi la KGB na mkewe akiwa mfanyakazi wa ndani ya ndege.

Poulsen: Morroco inafungika kwao.

$
0
0
IMG_5462
Kocha wa timu ya Taifa – Taifa Star Kim Poulsen na Nahodha wa Taifa Stars.
Na Mwandishi Maalumu,Marrkech, Morocco
Huku Timu ya Taifa Taifa Stars ikikabiliwa na mechi muhimu kesho (Jumamosi) dhidi ya Morocco kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia, Kocha Kim Poulsen amesema amejiandaa kucheza mpira wa kasi na wenye pasi za uhakika ili kuivuruga beki ya Morocco.
 
Kocha huyo ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha Morocco hawaupati mpira kwa urahisi.
 
“Wachezaji wako katika hali nzuri kabisa na wana ari ya kushinda mechi hii…tuna nguvu na tunajua namna ya kuwapiga Morocco,” alisema kocha huyo.
Alisema suala si mchezaji gani anaanza au washambulizi ni wangapi, bali ni kazi itakayofanyika uwanjani na ubora wa wachezaji wa Taifa Stars, inayofurahia udhamnini mnono wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
 
Alisema Morocco ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wa kulipwa lakini inafungika na Taifa Stars itaweka nguvu kuanzia mwanzo wa mechi.
“Unapocheza mechi kama hii inabidi uweke nguvu dakika za kwanza za mechi ili umpe mpinzani wakati mgumu kwa hivyo dakika za mwanzo zitakuwa muhimu sana katika mechi hii,” alisema.
 
Poulsen alisema baadhi ya watu nchini Morocco bado wanaamini kuwa ushindi wa mechi ya awali Jijini Dar es Salaam wa 3-1 dhidi ya Morocco ulikuwa wa kibahati tu. “Tunataka kuwadhihirishia kuwa tunaweza na Taifa Stars sio timu ndogo kama wanayodhani.”
 
Alisema mazingira ya kambi ni mazuri kabisa na wachezaji wote wako katika hali nzuri na tayari kwa mchezo huu.
 
“Katika hali ya kawaida ungetegemea hujuma nyingi ikiwemo hoteli mbovu, viwanja vibovu vya mazoezi na kadhalika lakini hapa ni tofauti kabisa…kwani mazingira ni mazuri,” alisema Poulsen.
 
Taifa Stars imeweka kambi katika Hoteli ya Pullman iliyoko nje kidogo ya Mji wa Marrakech.
 
Naye nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wamefanya mazoezi ya kutosha hasa ikizingatiwa kambi ilianzia Addis Ababa, Ethiopia ambako walicheza mechi ya kirafiki na Sudan na kutoa sare ya 0-0 kabla ya kuelekea Marrakech.
 
“Morocco ni timu kubwa, tunapaswa kuiheshimu lakini sio kuiogopa…tutapambana ili timu ipate matokeo,” alisema Kaseja.
 
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe, akizungumza kutoka Dar es Salaam alisema wao kama wadhamini wa Taifa Stars wana imani kubwa sana na Stars na wanaitaka iwape Watanzania raha kwa mara nyingine kwa kushinda mechi hiyo.
 
“Tumewaona wakifanya vizuri nyumbani kwa kushinda mechi tano mfululizo na sasa ni muda wa kupata ushindi nje,” alisema.
 
Stars iko katika kundi C pamoja na Ivory Coast, Morocco na Gambia. Kundi hilo linaongozwa na Ivory Coast yenye pointi 7, Tanzania 6, Morocco 2 na Gambia 1.
 
Mechi ya kesho itapigwa katika Uwanja wa Marrakech saa tatu usiku kwa saa za Morocco ambayo itakuwa saa tano kamili Tanzania.
 
Baada ya Morocco Stars itacheza na Ivory Coast nyumbani Jumapili ijayo na mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya Gambia Septemba mwaka huu.

Mzee Nelson Mandela hali mbaya alazwa tena hospitali kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.

$
0
0

Nelson Mandela-1484223

 Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela amelazwa tena hospitali kutokana na kujirudia tena kwa ugonjwa wa mapafu.

Afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94 ilianza kudhoofika na kubidi kupelekwa katika hospitali mjini Pretoria, ambapo taarifa zimesema yuko katika hali mbaya lakini imara.

Msemaji wa rais nchini humo Mac Maharaj amekaririwa akisema baadhi ya wanafamilia wake wamekuwa na karibu muda wote.

Amesema ni hali ambayo amekuwa nayo kwa kipindi kirefu na wanamatumaini kuwa na sasa pia itatibika kwa mafanikio.

Katika taarifa yake kutoka ikulu amesema rais huyo wa zamani yuko chini ya uangalizi wa madaktari bingwa ambayo wananya kila liwezekanalo kuhakikisha anapata nafuu na kurejea katika hali ya kawaida.

Taarifa hiyo ya ikulu imeongeza kuwa Rais Jacob Zuma kwa niaba ya Serikali na taifa anamuombea Madiba apone haraka.

Kanye West won’t be around during Kim Kardashian’s delivery.

$
0
0

Kim Kardashian, Kanye West

 

Reality TV star Kim Kardashian is reportedly upset with her boyfriend Kanye West’s decision to be away from the delivery room when she gives birth to their first child next month.

Kim, 32, is reportedly “devastated” that her rapper beau doesn’t want to be there to see their child come in to the world.

Kim, who had a baby shower with her close friends and family over the weekend, is concerned that Kanye will miss the birth altogether due to his album release and tour commitments.

The source added “She’s terrified he will miss the birth of their baby. She’s having a massive freak-out about it”.


Taifa Stars kushuka dimbani leo kuikabili Morocco ugenini.

$
0
0

1

 Picha juu na chini timu ya Taifa- Taifa Stars ikiwa katika hatua za mwisho za maandalizi ya mechi yao na timu ya Morocco (Lions of the Atlas).

7

6

 Taifa Stars inatupa karata yake ya pili ugenini kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia kwa leo (Juni 8 mwaka huu) kuikabili Morocco (Lions of the Atlas) kwenye Uwanja wa Grand Stade uliopo Marrakech, Morocco.

Ilipoteza ya kwanza ugenini dhidi ya Ivory Coast mwaka jana na kushinda mbili mfululizo nyumbani dhidi ya Gambia na Morocco.

Mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za Morocco ni ya pili kwa Stars katika uwanja huo ambapo mwaka juzi ilifungwa mabao 3-1.

 Washabiki wa Morocco wanaonekana kuikatia tamaa timu yao yenye pointi mbili tu nyuma ya Ivory Coast inayoongoza kundi hilo la C ikiwa na pointi saba, ikifuatiwa na Tanzania yenye sita. Huo ni mtazamo wa washabiki, lakini kwa upande wa timu inaonekana imepania kujichomoa katika nafasi za chini.

Kwa upande wa Kocha wa Stars Kim Poulsen amesema timu yake imepania mechi hiyo, lengo likiwa ni kuona inapata matokeo mazuri baada ya dakika 90 za mechi hiyo itakayokuwa chini ya refa Daniel Frazier Bennett wa Afrika Kusini.

Amesema timu yake itacheza kwa umakini na uangalifu kwa vile wanajua wapinzani wao wakicheza mbele ya washabiki wao watakuwa katika shinikizo za kushinda, jambo ambalo wamejiandaa kukabiliana nalo.

Kwa upande wa maandalizi, Kim amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadhamini wa timu hiyo Kilimanjaro Premium Lager wameiandaa vizuri kwani iko kambini kwa wiki tatu sasa na kupata mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan iliyochezwa wiki iliyopita nchini Ethiopia.

Stars iliifunga Morocco mabao 3-1 zilipokutana Machi 24 mwaka huu jijini Dar es Salaa. Lakini zilipokutana Marrakech mara ya mwisho mwaka 2011, Morocco iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Kim amesisitiza kuwa kikosi chake kimepania kufanya vizuri katika michuano hii ya mchujo ya Kombe la Dunia, na hiyo inathibitishwa na matokeo ya timu kadri inavyoendelea kucheza mechi za mashindano.

Moja ya mipango yetu katika mechi hizi za Kombe la Dunia ni kushinda nyumbani, hilo hadi sasa tumelifanya kwa asilimia 100. Lakini ili tukae vizuri zaidi tumekuja hapa Morocco kwa lengo la kupata matokeo mazuri, ingawa tunajua mechi itakuwa ngumi,” amesema kocha huyo raia wa Denmark.

Kwa hapa Marrakech mechi hiyo imekuwa haizungumzwi mara kwa mara, na kubwa ni kuwa Wamorocco wengi wanaamini kuwa timu yao ambayo hadi sasa ina pointi mbili haina nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano hiyo.

EU team of experts on Nuclear Safety and Security visits Tanzania.

Dereva wa bodaboda Singida afariki papo hapo baada ya kugongwa na basi la abiria.

$
0
0

01523

Mwili wa dereva wa bodaboda mjini Singida Hamisi Mkimbu, ukiwa barabarani baada ya kugongwa na basi la Mgamba na kufariki papo hapo.  Hamisi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 28 na 32, aligongwa katika barabara kuu ya Dodoma – Mwanza eneo la Kuvu Utemini mjini Singida.

01536

Pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Hamisi Mkimbu (bodaboda) baada ya kugongwa na basi la Mgamba T 759 AVJ lililokuwa linatokea Arusha kwenda Mwanza. Dereva Hamisi alifariki dunia papo hapo.

01528

Askari kanzu wakiubeba mwili wa dereva wa bodaboda Hamisi baada ya kugongwa na basi la Mgamba.

01534

Mwili wa dereva wa bodaboda Hamisi ukiwa umelazwa kwenye gari la polisi kwa ajili ya kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida.

01524

Baadhi ya wananchi wa Singida mjini, wakiangalia mwili wa dereva wa bodaboda Hamisi (haupo kwenye picha) baada ya kugongwa na basi la Mgamba. (Picha zote na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu.

Mfanyabiashara wa kusafirisha abiria kwa pikipiki (Bodaboda) mjini Singida Hamisi Mkimbu, anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka kati ya 28 na 32, amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Mgamba.

Kijana huyo alikumbana na dhahama katika barabara kuu ya Dodoma – Mwanza eneo la ‘kuvu’ kata ya Utermini mjini Singida.

Akizungumzia ajali hiyo shuhuda  Juma Rajabu, amesema wakati Mkimbu (marehemu) akiwa amefuata barabara hiyo kuu akitokea maeneo ya uwanja wa Namfua akielekea Bomani, kwa nyuma alikuwa anafuatwa kwa karibu na basi la Mgamba lenye namba za usajili T 759 AVJ lililokuwa linatokea Arusha linaelekea jijini Mwanza.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa Rajabu amesem “Mkimbu alipotaka kukata kona aingie barabara ndogo inayoanzia Kuvu kuelekea kituo cha mafuta cha Esso, kwa vile basi la Mgamba lilikuwa karibu naye sana,lilimgonga kwa nyuma na kusababisha kifo chake papo hapo”.

Rajabu amesema ni kawaida kwa magari makubwa hasa malori aina ya semi na mabasi, maderava wake wamejenga utamaduni wa kuwadharau waendesha pikipiki na kuwaona kama vile hawana haki ya kutumia barabara.

Akifafanua zaidi, amesema kuwa kutokana na dharau zao hizo, madereva hao huwa hawana tahadhari yo yote pindi wanapoiona pikipiki ipo barabarani.

Amesema “Hawajishughulishi kabisa kuangalia ‘indiketa’ za pikipiki wala kutoa nafasi na mwendesha pikipiki aendeshe kwa amani na usalama.

Mwendesha pikipiki atabanwa kwa makusudi hadi ajione kuwa yeye hapaswi kutumia barabara.

Huyu dereva kama angechukua tahadhari kwamba kuna chombo cha moto mbele yake, sitegemei kama tukio hilo lingetokea”.

Mkimbu ambaye inaelekea hakuvaa kofia ngumu, alipasuka kichwa  na ubongo ukamwagika barabarani na kuvunja damu nyingi.

Juhudi za kumpata Kamanda wa jeshi la polisi kuzungumzia ajali hiyo, zimegonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa Kamanda anaendelea na kikao.

Bondia Japhet Kaseba wa Tanzania leo kuzipiga na bondia Rasco Chimwanza wa Malawi.

$
0
0

Jafet kaseba akitunisha misuli mbele ya Anthony ruta ambaye alikuwa akisimamia zoezi zima la upimaji akisaidiwa na ibrahim kamwe 'bigright'Jafet kaseba akitunisha misuli mbele ya Anthony ruta ambaye alikuwa akisimamia zoezi zima la upimaji akisaidiwa na ibrahim kamwe 'bigright'

 

Japhet Kaseba akitunisha misuli mbele ya Anthony Ruta ambaye alikuwa akisimamia zoezi zima la upimaji akisaidiwa na Ibrahim Kamwe ‘Bigright’.

Bondia Japhet Kaseba jana alipima uzito tayari kumkabili mpinzani wake Rasco Chimwanza wa Malawi katika pambano la ubingwa wa kimataifa.

Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Anthony Ruta, Ibrahim Kamwe, Pendo Njau na Dkt. John Lugambila wa Muhimbili na kueleza kuwa mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani.

Kwa upande wake Japhet Kaseba amejinadi kumsambaratisha mpinzani wake katika raundi za mapema za mchezo huo.

Pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo Juma Fundi atazipiga na Hasan Kiwale (Moro Best), Josef Onyango kutoka Kenya atazipiga na Seba Temba wa Morogoro, huku Issa Omar (Peche Boy) atakapomvaa bondia mkongwe Juma Seleman na mapambano mengineyo mengi yatapigwa katika ukumbi DDC Magomeni Kondoa.

katika hali ambayo si yakawaida kwa vyama vya ngumi hapa nchini kuwa pamoja kikazi katika mapambano wanayoyasimamia, kwa pambano la leo Jumamosi itakuwa tofauti kwani baadhi ya maofisa wa chini wa vyama vya ngumi kusimamia mapambano kwa pamoja na kuua tofauti zao na kujirudi kuwa wao ni wamoja katika michezo.

Hoyce Temu akonga nyoyo za washiriki wa semina ya ‘How To Find Your Destiny’.

$
0
0

IMG_0103

Mwendesaji wa semina ya “How To Find Your Destiny”  Hoyce Temu akisikiliza utambulisho kutoka kwa washiriki waliohudhuria semina hiyo ambao baadhi yao ni wajasiriamali, waajiriwa wa serikali, Mentors na wanafunzi wa vyuo. Semina hiyo  imefanyika kwenye Taasisi ya Mara Foundation ya jijini Dar.

IMG_0131

Pichani juu na chini ni Mwendeshaji wa semina ya “How To Find Your Destiny”  Hoyce Temu aki-share experience ya maisha yake mpaka hapo alipofika baada ya kupitia vikwazo vingi, kuvuka mabonde na malima wakati wa semina hiyo.

IMG_0133

IMG_0121

Pichani juu na chini ni Washiriki wa semina ya “How To Find Your Destiny” wakifuatilia kwa umakini shuhuda na mifano mbalimbali ya maisha iliyokuwa ikitolewa na Mwendeshaji wa Semina hiyo Hoyce Temu(hayupo pichani).

IMG_0130

IMG_0171

Mwendeshaji wa Semina ya  “How To Find Your Destiny”  Hoyce Temu akigawa kitabu chake kinachoelezea historia ya maisha yake kinachoitwa “Nayakumbuka Yote” ambacho kinauzwa katika maduka mbalimbali ya vitabu jijini Dar na Pesa inayopatikana katika mauzo hayo asilimia 80 inakwenda kulipia ada za shule kwa wasichana ambao ni mayatima na asilimia 20 inakwenda kwa mchapishaji.

IMG_0175

Mmoja wa washiriki akimpongeza Hoyce Temu kwa ujasiri aliokuwa nao na mateso aliyopitia katika maisha yake mpaka kufikia hapo alipo.

IMG_0184

Hoyce Temu akisaini autograph kwa mmoja washiriki.

IMG_0195

Hoyce Temu akishow love na Mmiliki wa Beutylicious Saloon iliyopo Mikocheni B Irene Juliet Mbuya.

IMG_0194

Pichani juu na chini ni Baadhi ya washiriki wakipata picha ya ukumbusho na Mrembo wa zamani aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu.

IMG_0188

Vijana jijini Dar es Salaam wamepata fursa ya kushiriki katika semina iliyoandaliwa na Mikono Business Consult  kwa ajili ya kuwapa hamasa na kuwataka wasikate tamaa ili wajipange na kuangalia nini wanachotaka kukifanya katika maisha yao.

Semina hiyo iliyoendeshwa na Miss Tanzania wa zamani na Communication Analyst wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Hoyce Temu ilifahamika kwa jina la “How To Find Your Destiny” imeonekana kuwavutia washiriki waliohudhuria kutoka sehemu mbalimbali.

 

Dondoo na Tetesi za uhamisho na usajili wa wanasoka Kimataifa.

$
0
0

495506628_96450c6696

Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amepewa ruhusa kuendelea na mipango ya kumyakua mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney. Mtendaji Mkuu wa The Gunners Ivan Gazidis amesema klabu hiyo itamudu gharama za mchezaji huyo wa kimataifa.

Klabu ya Monaco ya Ufaransa ambayo tayari imeshatumia zaidi ya Paundi milioni 100 kwa ajili ya wachezaji wapya kipindi hiki cha kiangazi, iko tayari kumuwinda kapteni wa Chelsea John Terry. Monacoinaamini kuwa kitita cha takriba paundi milioni 7 kinatosha kuwashawishi The Blues kumuachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32.

Klabu ya Livapool inapanga mikakati thabiti ya kumchukua mshambuliaji wa Manchester City Carlos Teves mwenye umri wa miaka 29, ili kuziba pengo la Luis Suarez.

Meneja mpya wa Manchester United David Moyes amepanga kumfanya beki wa kulia wa klabu ya Penarol ya Uruguay kuwa wa kwanza kutia saini Old Trafford. Mchezaji huyo Guillermo Varela mwenye umri wa miaka 20 anapatikana kwa kitita cha paundi milioni 1.2.

CCM Dar yafanya Mazungumzo na Ujumbe wa Chama cha Kikomunisti chaVietnam.

$
0
0
2
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (aliyesimama) akifunga mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramdahani Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam, kwenye Ofisi za CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo.

Na Pius Ntiga, UHURU FM

Chama Cha Kikomunisti Cha Vietnam-CVP, kimekitaka Chama Cha Mapinduzi-CCM, kutoogopa kuwafukuza uanachama wake wasio na nidhamu ambao hawazingatii maadili na kanuni za Chama kilichpo Madarakani.

          Pia Chama hicho cha CVP kimesisitiza kuwa ni bora kuwa na wanachama wachache kuliko kuwa na wanachama wengi wasio na nidhamu.

          Kauli hiyo ya Chama cha Kikomunisti Cha Vietnam, imetolewa leop Juni, 8, 2013 na Kiongozi wa Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Bwana HOANG BINH QUAN wakati wa mazungumzo na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Mkoa wa Dar es salaam ambao umeongozwa na Mwenyekiti wake Ramadhan Madabida.

          Katika mazungumzo hayo, Bwana QUAN pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa Chama cha siasa kudumisha nidhamu ndani ya Chama na kuachana kabisa na kasumba ya kuwa na wanachama wengi huku miongoni mwao wakiwa ni wasaliti wakubwa ndani ya Chama.

          Kwa sababu hiyo Bwana QUAN akakiomba Chama Cha Mapinduzi ambapo katika mazungumzo yao yalihuidhuliwa pia na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE kutowaonea haya wanachama wasaliti ndani ya Chama.

          Hata hivyo Chama Cha Mapinduzi-CCM kupitia kwa Katibu wake Mkuu ABDULRAHMAN KINANA, tayari kilishatoa kauli kama hiyo ya kuwa ni bora kuwa na wanchama wachache wenye nidhamu kiliko kuwa na wanachama wengi wasio na nidhamu.

          Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida ameuambia ujumbe wa Chama hicho cha Kikomunisti Cha Vietnam kuwa CCM itaendelea kudumisha uhusiano wa siku nyingi na Chama hicho huku akisistiza umuhimu wa wananchi wa Vietnam kuja kuwekeza nchini hasa katika Mkoa wa Dar es salaam kutokana na fursa mbalimbali zilizopo.

          Pia pamoja na mambo mengine amezungumzia haja ya vyama hivyo viwili vya CCM pamoja na CVP kubadilishana wanachama kwa kwenda kujifunza namna mbalimbali za Kiuongozi ndani ya vyama hivyo.

          Madabida ameainisha maeneo machache ya uwekezaji katika jiji la Dar es salaam kuwa ni pamoja na eneo la uvuvi kupitia Bahari ya Hindi, kilimo pamoja na  sekta ya umeme hivyo akaomba wawekezaji kutoka Vietnam kuja kuwekeza Tanzania.

          Akishukuru kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi kuhusiana na ugeni huo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE amesema ujio wa viongozi hao umefungua ukuraa mpya wa ushirikaino katika Nyanja mbalimbali za kisiasa hasa ikizingatiwa historia ya muda mrefu kati ya CCM na CVP.

          Katika kusisitiza umuhimu wa ushirikiano huo Nape amesema CCM daima itaendelea kushirikiana na Chama cha CVP kutokana na misingi iliyoachawa na Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Rais wa Kwanza wa Vietnam HO CHI MIHN.

          Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Afisa wa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa CCM Makao Makuu Bi.Juliana Chitinka, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ernest Charle, Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Silvester Mrope pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni Salum Madenge.

          Ujumbe huo wa Chama Cha Kikomunisti Cha Vietnam-CVP, umemaliza ziara yake ya kichama hapa nchini na ulitarajiwa kuondoka kurejea nchini kwao Vietnam leo mchana.

 Mjumbe wa Chama Cha bKimomunisti cha China, akimpa zawadi Madabiba baada ya mazungumzo yao.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine.


Magdalena Olotu alikwaa taji la Redd’s Miss Kigamboni 2013.

$
0
0

IMG_0227

 Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akiwa ameambatana na Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya wakiwasili ukumbini.(Picha zote na Zainul Mzige wa Dewjiblog).

IMG_0233

Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akisalimiana na  Aliyewahi kuwa Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu (Somo wa washiriki wa Redd’s  Miss Kigamboni 2013). Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel.

IMG_0234

Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel mara baada ya kuwasili ukumbini.

IMG_0244

Meza ya Majaji ikiongozwa na Chief Judge Mwandaaji wa Miss Temeke Bw. Benny Kisaka (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa CXC Tours and Safari Bw. Charles Hamka ( wa pili kulia), Mratibu wa Miss Ilala Juma Mabakila (Kushoto) na Mkuu wa Radio France nchini Bw. Victor Willy (kulia).

IMG_0284

Mwandaaji wa mashindo ya Redd’s Miss Kigamboni 2013 Angella Msangi akiteta jambo na Chief Judge wa mashindano hayo.

IMG_0307

Picha juu na chini ni Washiriki 11 wa Redd’s Miss Kigamboni wakifungua shindano hilo kwa show ya aina yake.

IMG_0319

IMG_0203

Wanenguaji wa Bendi ya FM ACADEMIA maarufu kama Wazee wa Ngwasuma wakitoa burudani wakati wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Kigamboni 2013 lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni jijini Dar.

IMG_0369

Pichani juu na chini washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni wakipita jukwaani mavazi ya ubunifu.

IMG_0372

IMG_0403

Washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni 2013  ndani ya Beach Wear.

IMG_0433

Mmoja wa majaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa CXC Tours and Safari Bw. Charles Hamka akitangaza majina ya warembo waliofanikiwa kutinga tano bora.

IMG_0450

Washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni waliofanikiwa kutinga tano bora.

IMG_0485

 Aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye pia ni Somo wa washiriki wa Redd’s  Miss Kigamboni 2013 akiwauliza maswali washiriki  waliofanikiwa kutinga tano bora kwenye shindano hilo.

IMG_0472

Washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 wakijibu maswali.

IMG_0506

Wadau wa tasnia ya urembo wakishangilia baadhi ya washiriki waliokuwa wakijibu maswali yao bila kutetereka.

IMG_0526

Miss Kigamboni 2012 Edda Slyvester anayemaliza muda wake akisubiri kukabidhi taji kwa Redd’s Miss KIgamboni 2013.

IMG_0555

Miss Kigamboni 2012 Edda Slyvester aliyemaliza muda wake akimvisha taji mshindi wa shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (aliyeketi) wakati wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni jijini Dar.

IMG_0566

Mshindi wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Latifa Mohamed( wa pili kushoto) na Mshindi wa tatu Irene Rajab ( wa pili kulia) pamoja na mshindi wa nne na wa tano.

IMG_0570

IMG_0588

Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akitoa nasaha zake kwa mshindi wa taji la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu mara baada ya kuibuka kidedea wa taji hilo ambapo amemtakia Baraka zote kuiwakilisha vyema Kigamboni.

IMG_0596

Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 500,000/mshindi wa taji la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu iliyotoka mfukoni kwa Mbunge huyo.

IMG_0601

Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya akikabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 250,000/ kwa mshindi wa tatu wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 Irene Rajab.

IMG_0605

Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel katika pozi na mshindi wa pili wa shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Latifa Mohamed mara baada ya kumkabidhi zawadi ya fedha taslim shilingi 300,000/.

IMG_0612

Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu katika pozi na kitita chake cha fedha taslim shilingi 500,000/ zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile

IMG_0606

Raia wa kigeni kutoka China aliyehudhuria shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 akichukua picha ya ukumbusho ya mshindi wa taji hilo.

IMG_0586

Mwandaaji wa shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Angella Msangi (kulia) na Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng’itu pamoja na Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya (kushoto) wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi.

IMG_0220

 Raia wa Kigeni kutoka china ndani Redd’s Miss Kigamboni 2013.

IMG_0222

 VIP Table… Alikuwepo Bw. William Malecela a.k.a LEMUTUZ, Katibu Mkuu wa kamati ya Miss Tanzania, Bw. Bosco Majaliwa, Aliyewahi kuwa Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu (Somo wa washiriki wa Redd’s  Miss Kigamboni 2013), Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel wakati wa shindano la kumtafuta Redd’s Miss Kigamboni lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Navy Beach Kigamboni.

IMG_0238

Picha juu na chini ni baadhi ya Wadau wa tasnia ya masuala ya Urembo kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar waliohudhuria shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013.

IMG_0239

IMG_0517

IMG_0508

Nyomi ya Ukweli… Clouds Tv walikuwepo kuhakikisha shindao hilo linaruka Live.

IMG_0533

Aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye pia ni Somo wa washiriki wa Redd’s  Miss Kigamboni 2013 akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa.

IMG_0615

Wadau wa tasnia ya Urembo wakishow love mara baada ya shindano hilo kumalizika.

Dr. Asha Rose Migiro aongoza matembezi ya Hisani kuchangia fedha katika Kutokomeza Ugonjwa wa Fistula na kuzuia Vifo vya Mama na Mtoto.

$
0
0

126

Dr. Asha Rose Migiro katikati Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa Chama cha Mapinduzi CCM akiwasili katika hoteli ya Golden Tulip mahali ambapo matembezi ya hisani kuchangia fedha kwa ajili ya kuapambana na Ugongwa wa Fistula na kuzuia vifo kwa mama na mtoto yamefanyika jijini Dar es salaam na kushirikisha taasisi na mampuni mbalimbali nchini, matembezi hayo yameandaliwa na benki ya Barclays, kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Barclays Kihara Maina na kushoto ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa kampuni ya Montage ambayo ndiyo imeratibu matembezi hayo

2

Dr. Asha Rose Migiro Kushoto Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa Chama cha Mapinduzi CCM akishiriki mazoezi kabla ya kuanza kwa matembezi hayo leo asubuhi kutoka kulia ni Dr. Aloyce Nzuki Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii TTB, Abdulkarim Shah Mbunge wa Mafia na mjube wa bodi ya wakurugenzi ya TTB Kihara Maina Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays

3

Dr. Yasin akiongoza mazoezi kabla ya kuanza kwa matembezi hayo leo asubuhi.

4

Dr. Asha Rose Migiro Kushoto Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa Chama cha Mapinduzi CCM akishiriki mazoezi kabla ya kuanza kwa matembezi hayo leo asubuhi kutoka kulia ni Dr. Aloyce Nzuki Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii TTB, Abdulkarim Shah Mbunge wa Mafia na mjube wa bodi ya wakurugenzi ya TTB, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TTB Baozi Charles Sanga na Kihara Maina Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays.

5Bendi ya polisi ikiongoza matembezi hayo 6Matembezi yakiendelea 7Yalipitia katika mitaa mbalimbali ya Oysterbay jijini Dar es salaam na kuishia Golden Tulip 8

Yakielekea kumalizika rasmi.

9

Ikawa ni kupasha mwili baada ya kumalizika kwa matembezi hayo.

10

Mmoja wa walemavu alishiriki bega kwa bega katika matembezi hayo hapa akiwa anafanya mazoezi.

Taifa Stars yafa kiume Morocco.

$
0
0

12

 

Kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika picha ya pamoja.

1 (1)

-Yafungwa mabao 2-1

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Marakech mjini hapa na wenyeji Morocco, katika mchezo wa Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani.

Hadi mapumziko, Morocco walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Abderazak Hemed Allah dakika ya 37, baada ya yeye mwenyewe kujiangusha kwenye eneo la hatari baada ya kugongana na Aggrey Morris.

Morris alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya hapo na Stars wakabki pungufu.

Morocco ndiyo waliocheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza wakishambulia zaidi upande wa kulia alipokuwa akikimbiza Belhanda

Dakika ya 25 Thomas Ulimwengu alifanya kazi nzuri ya kumtoka beki, lakini shuti lake likadakwa na kipa. 

5

Kocha Kim Poulsen aliwapumzisha kwa mpigo washambuliaji Mrisho Ngassa na Ulimwengu dakika ya 44 na kuwaingiza beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo Khamis Mcha ‘Vialli’.

Kipindi cha pili Morocco walirejea na moto tena, wakiishambulia zaidi Stars iliyoonekana kudhoofika na katika dakika ya 50 Youssef El Arabi  akafunga  bao la pili kiulaini baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania na kubaki na kipa Juma Kaseja.

Hata hivyo, shambulizi la kushitukiza liliipatia Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager bao la kwanza dakika ya 61 lililofungwa na Amri Kiemba kwa shuti la mbali kutoka wingi ya kushoto.

3

Morocco waliendelea kutawala mchezo na Stars walikuwa wakifanya mashambulizi ya kushitukiza ambayo kwai kiasi fulani yalikuwa ya matumaini.

Dakika ya 82 Kim alimpumzisha Vialli na kumuingiza John Bocco ‘Adebayor’ ambaye aliongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.  

Kwa matokeo hayo, Stars inabaki na pointi zake sita baada ya kucheza mechi nne, kushinda mbili nyumbani na kufungwa mbili zote ugenini, nyingine ikiwa dhidi ya Ivory Coast.

Lakini Stars inabaki nafasi ya pili mbele ya Morocco yene pointi tano sasa, wakati Ivory Coast wanaongoza kwa pointi zao saba kabla ya matokeo ya mechi na Gambia leo.

2

 

kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Kevin Yondan, Aggrey Morris, Frank Domayo, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mchadk44/John Boccodk82, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Nadir Haroub dk44.

Stars bado inashika nafasi ya pili katika Kundi c na pointi 6 huku Ivory Coast ikiongoza kwa pointi 10 baada ya kuifunga Gambia 3-0 jana wakati Morocco ni wa tatu na pointi 5 na Gambia pointi 2.

Taifa Stars itacheza na Ivory Coast Jumapili ijayo jijini Dar es Salaam wakati Gambia itacheza na Morocco.

18

Watanzania wanaoishi Morocco wakishangilia timu ya Taifa Stars wakati wa mechi na Morocco usiku wa kuamkia leo.

Angalia Matukio ya Shida ya Maji Kata ya Kishapu.

$
0
0

Na Thehabari.com, Kishapu

Wanasema maji ni uhai, kinyume chake bila maji hakuna uhai wa mwanadamu na hata wanyama.

Kimsingi kauli hii inaonesha umuhimu wa maji katika maisha ya kila siku ya binadamu na hata viumbe wengine.

Shughuli nyingi zinazofanywa na mwanadamu kila siku zinategemea uwepo wa maji. Matumizi ya maji kwa shughuli za binadamu hayaepukiki. Na hata katika mwili wa binadau ni muhimu zaidi,  kama huto yaitaji maji kwa kunywa utayahitaji kwa kuoga na usafi wa shughuli nyingine.

Kwa mantiki hiyo hali yoyote ya upatikanaji ngumu ya upatikanaji wa maji unaathiri maisha ya kila siku ya mwanadamu. Shida ya huduma ya maji eneo fulani huweza kuchangia ugumu wa  maisha kiasi fulani.

Shida ya maji maeneo mengine huweza kupunguza shughuli za uzalishaji mali, hii ni kutokana na muda mwingi kupotezwa na jamii kwa ufuatiliaji wa maji hasa maeneo ya vijijini.

Hali kama hii ya shida ya huduma ya maji ndiyo inayowakumba wananchi wa vijiji anuai vya Kata ya Kishapu, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga. Kata ya Kishapu ina vijiji nane yaani Mhunze, Lubaga, Isoso, Mwanuru, Migunga, Mwamagembe, Mtaga, na Kishapu yenyewe.

Japokuwa vijiji vingi vina shida kubwa ya huduma za maji, lakini hali ya ugumu wa upatikanaji huduma hizo hutofautiana kutoka kijiji kimoja hadi kingine. Kati ya vijiji vyote nane vijiji vinne ndio vyenye shida ya maji zaidi. Vijiji hivyo ni pamoja na Lubaga, Isoso, Mwanuru na Kishapu yenyewe.

Zifuatazo ni picha anuai zikionesha wananchi wanavyoangaika kutafuta huduma za maji vijiji hivyo.

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kishapu wakichota maji kwenye mto

 Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kishapu wakichota maji kwenye mto.

Haya ni maji yaliotuwama, si salama lakini wakazi hulazimika kuyatumia kutokana na shida ya huduma hiyo.

Haya ni maji yaliotuwama, si salama lakini wakazi hulazimika kuyatumia kutokana na shida ya huduma hiyo.

Heka heka za utafutaji maji eneo la Mto Tungu.

Heka heka za utafutaji maji eneo la Mto Tungu.

Wanyama anuai wakinywa maji kwenye chanzo cha maji ambacho hutumiwa pia na wanakijiji.

Wanyama anuai wakinywa maji kwenye chanzo cha maji ambacho hutumiwa pia na wanakijiji.

Mchuuzi wa maji Kijiji cha Mhunze akichota maji kwaajili ya kuuza. Dumu moja huuza wastani wa sh 500.

Mchuuzi wa maji Kijiji cha Mhunze akichota maji kwaajili ya kuuza. Dumu moja huuza wastani wa sh 500.

Mmoja wa waandishi wa habari kutoka kituo cha Clouds FM, Aziz Kindamba akinywa maji kwenye kisima cha muda.

Mmoja wa waandishi wa habari kutoka kituo cha Clouds FM, Aziz Kindamba akinywa maji kwenye kisima cha muda.

Mmoja wa waandishi wa habari kutoka Thehabari.com akinywa maji kwenye kisima cha muda.

Mmoja wa waandishi wa habari kutoka Thehabari.com akinywa maji kwenye kisima cha muda.

Mashimo haya ni visima vya muda ambavyo kwa sasa vimekauka katika eneo la Mto Tungu.

Mashimo haya ni visima vya muda ambavyo kwa sasa vimekauka katika eneo la Mto Tungu.

Mwanafunzi akifua eneo la chanzo cha maji Kishapu

Mwanafunzi akifua eneo la chanzo cha maji Kishapu.

Wanawake nyumbani ndio watafutaji zaidi wa maji

Wanawake nyumbani ndio watafutaji zaidi wa maji.

Wakati wananchi wengine wanachota maji wengine hufua eneo hilo.

Wakati wananchi wengine wanachota maji wengine hufua eneo hilo.

Mkutano wa Wahariri wa vyombo vya Habari na TANAPA waendelea mkoani Iringa.

$
0
0

136

Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Allan Kijazi akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa washiriki wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TANAPA unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Maada mbalimbali zinawasilishwa leo ikiwa ni pamoja na Masuala ya Utalii ndani ya hifadhi, Miradi ya ujirani mwema na Ulinzi katika mbuga.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA.

2

Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Mubnge wa jimbo la Iringa mjini Mchunagji Peter Msigwa akitoa mada katika mkutano huo wakati wa majadiliano kuhusu utalii katika hifadhi za TANAPA kulia ni Mkurugenzi wa Tanapa na Kushoto ni Dr. Ayoub Rioba na mstari wa nyuma kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli na kushoto ni Meneja uhusiano wa TANAPA Bw. Pascal Shelutete.

3

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli akizungumza katika mkutano huo unaoendelea mjini Iringa leo.

4

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli akisisitiza jambo wakati akichangia mada katika mkutano huo unaoendelea leo.

5

Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Ndugu Charles Misango akiuliza swali katika mkutano huo.

6

Dr. Ayoub Rioba akiendesha majadiliano katika mkutano huo.

7

Mwandishi wa habari Antonio Nugas kutoka Radio Clouds kushoto akiwa pamoja na washiriki wengine katika mkutano huo.

8

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo.

9

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo.

10

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo.

Viewing all 1758 articles
Browse latest View live