Mkuu wa Huduma za Rejereja za Kibenki wa Benki ya NBC Tanzania, Mussa Jallo (wa pili kushoto) akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya benki hiyo ambayo washindi wanne walikabidhiwa pikipiki mpya aina ya Honda. Hafla hiyo ilifanyika pamoja na uchezeshwaji wa droo ya pili katika Tawi la NBC Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe, Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Chiku Saleh.
Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya NBC Weka Upewe, Festo Mukerebe (kulia) akionyesha ufunguo wa pikipiki aina ya Honda, mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Kanda wa NBC, Rachel Mwalukasa (kushoto) katika hafla hiyo iliyofanyika katika Tawi la Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
.Waendesha droo ya pili kwenye tawi la Ubungo
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imefanya droo yake ya pili ya promosheni ya “weka upewe” huku wakigawa zawadi kwa washindi wa kwanza wa droo hiyo amabyo ilifanyika katika mikoa mitatu ya Tanzania bara.
Droo hiyo iliyofanyika katika tawi la Ubungo, ilikwenda sambamba na shughuli ya kutoa zawadi kwa washindi wa droo ya mwanzo wa promosheni ya “weka upewe” ambapo wateja Chris Peter Maina , Edna Ndumbaro, Walter J Nyaki na Festo E Mukerebe walipata zawadi zao za Honda Pikipiki, wakati Michael C Kipingu kutoka Moshi na Saad A Abasi kutoka Makambako walipata jenereta za nguvu.
Akizungumza wakati wa kutoa zawadi hizo jijini Dar es Salaam kwa washindi , Mkuu wa Huduma za Reja Reja, Mussa Jallow alisema, “Sisi kama taasisi ya fedha tunapata faraja kuona wateja wetu leo hii wanapata zawadi na wana kila sababu ya kufurahi kubadilisha maisha kupitia benki ya watu ya NBC,”
” Zawadi hizi na makabidhiano haya leo kwa njia moja au nyingine itabadilisha maisha ya wateja wetu na ni njia ya kutatua matatizo yao ya usafiri, masuala ya nishati au kuongeza mapato ya ziada na kusaidia familia zao ,” aliongeza
Akitoa maoni yake juu ya droo ya pili , Jallow alisema, ” Ni hatua nzito ambayo tuna mafanikio na sisi ni sehemu ya maisha ya watanzania na tunafanya droo ya pili kwa ajili ya kukuza biashara za wateja wetu kupitia promosheni ya Weka Upewe .”
Kwa upande wake Mkuu wa Wateja Wakubwa na Madeni, Andrew Massawe alisema kwamba benki ya NBC itaendelea kuboresha huduma zake na kuja na bidhaa mpya kwa ajili ya watanzania na aliwataka wateja kuendelea kujitokeza kwa wingi katika kufungua akaunti ili waweze kujishindia zawadi kem kem.
“Sisi tunafarijika kuona wateja wetu wakiendelea kupata zawadi zao na kukuza biashara au mitaji yao katika shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato na kufaidika na punguzo la riba kupitia promosheni hii ya weka upewe,”
“Sisi tunahamasisha wateja wetu wote kujiunga katika promosheni kwa kufungua akaunti na kwa sababu hata kama hukupata zawadi bado unaweza kufurahia viwango bora kwa huduma. ” Alisisitiza
Baadhi ya washindi kutoka mikoa mingine Tanzania walipokea zawadi na makabidhiano yalifanyika jijini Dar es Salaam.
Weka upewe promosheni ilizinduliwa Oktoba pamoja na Huduma kwa Wateja wa mwezi , itaendelea mpaka mapema Januari mwaka 2014, ambapo jumla ya washindi kumi na nane watapata zawadi zao za Pikipiki na jenereta, na moja ataondoka na gari aina ya 2013 Suzuki Swift.
Ili kuingia katika droo mteja anahitaji kufungua akaunti na akaunti ya Malengo Akaunti au kufungua na amana kwa mwaka mmoja na Akaunti ya Amana ya kudumu na kwa wateja wote wapya na wazamani.