Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw. Sylvester Manyara (katikati) akichezesha droo ya nne ya Pambika na Samsung huku akishuhudiwa na Msimamizi toka Bodi ya michezo ya kubahatisha Bw. Emmanuel Ndaki (Kushoto) huku kulia ni Mratibu wa Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew.
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzaia Bw Sylvester Manra akiongea na mmoja ya washindi wa droo ya nne ya promosheni ya Pambika na Samsung mara baada ya kuchezesha droo hiyo ya nne. Jumla ya washindi 15 wamezawadiwa bidhaa mbalimbali toka Samsung katika droo ya nne mara baada ya kununua bidhaa halisi za Samsung na kuisajili.
Katika kuhakikihsa elimu ya huduma ya kusajili bidhaa za Samsung muhimu kwa Watanzania inasamabaa kwa haraka zaidi, Samsung Tanzania ilizindua promosheni kabambe katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka inayojulikana kama Pambika na Samsung itakayodumu mpaka Desemba 23, 2013. Promosheni hiyo inalenga kuhamasisha wateja kununua bidhaa halisi na kuzisajili kasha kuzawadiwa katika droo za kila wiki na droo kubwa ya mwisho wa promosheni.
Akizungumza wakati wa droo ya nne ya kila wiki ya Pambika na Samsung, Bw. Sylvester Manyara Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania amesema kwamba Samsung inadhamira ya dhati katika kulinda haki za mteja na kumlinda kutokana na bidhaa feki ambazo zipo kila kona kwa sasa. “Wateja wote wana haki ya kujua kuhusu umiliikaji wa bidhaa zao wakati wa kununua. Ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa Samsung tunajitolea kulinda haki za wateja kwa kuwapa wateja wetu jukwaa la kufurahia uamuzi wao wa kununua bidhaa halisi” alisema Bw. Manyara.
Droo ya nne imetoa washindi 15 wengine ambao wamepokea bidhaa mbalimbali toka Samsung kama Jokofu lenye dhamana ya miaka 10 toka Samsung, Luninga ya LED 32’, Kompyuta mpakato, Jiko la kupashia chakula, Muziki wa nyumbani pamoja na deki za DVD toka Samsung. Jumla ya wateja 60 kutoka mikoa mbalimbali tayari wameshapatikana.
Badhii ya washindi wa wiki hii ni Hasmin Karim (25) wa Dar es salaam mshindi wa Mashine ya kuoshea nguo, Devotha Richard, (20) mwanafunzi wa TIA mbeya, Walter Milanzi (32) wa Dodoma, James Kedela (53) wa Mwanza na Martha Mushi (27) wa Moshi wote wakijishindia deki ya DVD.
Hii ni aina nyengine ya huduma iliyoletwa na Samsung ili kulinda haki za wateja na kuwalinda kutokana na madhara ya kununua bidhaa feki. Pambika na Samsung inawazawadia wale wote wanaonunua na kusajili bidhaa halisi za Samsung kila wiki kabla ya kutolewa kwa zawadi kubwa ya gari jipya la Mitsubishi Double Cabin itakayokuwa imesheheni bidhaa zote zinazotoka kila wiki ambapo mteja mmoja mwenye bahati atajinyakulia hapo Desemba 23, 2013.