Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Hoyce Temu alamba Nondozzz ya shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma St. Augustine University

$
0
0

Picture 019

Aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akipozi mara baada ya kulamba Nondozzz ya  shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine jijini Mwanza.

Picture 018

Hoyce Temu akipata Ukodak na Mdau wa tasnia ya habari nchini.

Picture 013

 Hoyce Temu katika pozi na marafiki zake mara baada ya kulamba Nondozz.

Picture 026

Pongezi pia ziende kwa Dada Lulu Musa Afisa Uhusiano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kwa kulamba Nondozz ya shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma katika chuo cha St. Augustine University kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa Juma.

Picture 045

Mbali na kula Nondozz kwenye siku hiyo maalum Hoyce Temu ambaye pia ni Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania aliamua kufanya mahojiano na baadhi ya wahitimu kwa ajili ya kipindi chake.

Picture 055

Mlimbwende Hoyce Temu akizungumza na mwandishi wa habari wa ITV  kuhusiana na taalum aliyoipata itakavyoweza kuboresha utendaji wake kazini pamoja na kuendelea kuisaidia jamii inayomzunguka kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania.

Picture 070

Mwanandishi wa habari wa kituo cha ITV Shaban Tole akimpongeza Hoyce Temu.

Picture 078

Hoyce Temu katika picha ya kumbukumbu na marafiki.

Picture 071

Hoyce Temu akiondoka eneo la tukio na furaha isiyo na kifani.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758