Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

TIB kuanza uwekezaji kwenye miundombinu ya Reli

$
0
0

8188052588_9b61c95ad7_h

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya TIB, Peter Noni (Picha na Maktaba).

-Kusudio ni kuharakisha maendeleo ya usafirishaji wa mizigo na mawasiliano

Na Damas Makangale, Mbeya

BENKI ya Maendeleo Tanzania (TIB) inakusudia kuanza uwekezaji katika miradi mikubwa kama vile ujenzi wa miundombinu ya reli, umeme, barabara na mawasiliano ili kuisaidia Serikali kuongeza kasi ya kuboresha mtandao wa miundombinu ya kiuchumi.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya TIB, Peter Noni wakati wa sherehe ya uzinduzi wa makao makuu ya Benki hiyo Kanda  ya Nyanda za Juu Kusini iliyofanyika Jijini Mbeya.

“Benki yetu kwa sasa inajipanga kuanza uwekezaji katika miradi mikubwa ya miundombinu ya kiuchumi. Miradi hiyo ni kama vile reli, barabara, umeme na mawasiliano,” alisema Noni.

Alisema kuwa ili kufanikisha azma hiyo, watashirikiana na benki nyingine za maendeleo nje ya nchi ambazo zina ushirikiano na TIB. Akazitaja baadhi ya benki ambazi TIB inakusudia kushirikiana nazo kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu nchini kuwa ni DBSA, IDC, BNDES na CDB.

 Alisema mbali na benki hiyo kujikita na miradi hiyo ya  ujenzi wa miundombinu, pia inakusudia kuwasaidia waqnanchi wa kima cha chini hasa waishio vijijini ili waweze kujikwamua nna umasikini.

Alisema kwa kuanzia  mwaka wa 2013, Benki ya TIB imejipangia kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi Bilioni 379, ambazo zitaiingizia benki hiyo faida isiyopungua shilingi milioni 16 kabla ya kulipa kodi ya Serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIB, Prof. William Lyakurwa alisema kuwa Baada ya Serikali kuamua kuifufua TIB, imeamuliwa kuwa sasa benki hiyo itajiendesha kwa mfumo wa makampuni tazu yanayotegemeana ndani ya benki hiyo.

Alisema Kampuni ya kwanza itakuwa ni TIB Development Bank Ltd na kampuni ya pili itajulikana kwa jina la TIB Corporate Finance Bank Ltd ambayo itakuwa benki ya kibiashara, mahususi kwa ajili ya wateja wa benki ya maendeleo.

Alisema kuwa kampuni ya tatu itakuwa ni TIB Railimali Ltd ambayo kazi yake itakuwa ni udalali wa hisa za makampuni mbalimbali akisema kuwa mfumo huo unatarajiwa kuboresha ufanisi katika shughuli za kibenki na hivyo kutoa huduma bora kwa wateja wake.

Mgeni Rasmi wa Sherehe hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema kuwa nia ya Serikali ni kuiwezesha TIB kuwa taasisi imara ambayo italeta chachu ya uwekezaji katika viwanda vya kusindika mazao ya wakulima, wavuvi na wafugaji na miradi mingine ya uzalishaji ili kuwawezesha wananchi kupata masoko ya uhakika ya mazao yao na hivyo kujiongezea kipato.

Alisema kuwa ili wananchi waweze kunufaika na jasho lao litokanalo na  kilimo, ni lazima taifa liachane na mfumo wa kuuza mazao ghafi nje ya nchi badala yake mazao hayo yawe yanasindikwa hapa nchini  kabla ya kuuzwa nje ya nchi ili kuyaongezea thamani.

Alisema kuwa ili kuonyesha mfano, hivi sasa Serikali mkoani Mbeya inaandaa program ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ili kanda hiyo ianze kuzalisha matunda, mboga mboga na maua kwa ajili ya masoko ya mazao hayo nje ya nchi.

Mkuu huyo wa mkoa pia alitoa wito kwa wananchi kujenga tabia ya kurejesha mikopo ili taasisi zinazojihusisha na utoaji wa mikopo hiyo ziweze kujiimarisha na kuendelea kuhudumia watu wengi zaidi.

Benki ya Maendeleo nchini (TIB) ilizinduliwa upya na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 30, 2010.

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles