KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Maafisa Mawasilino Serikalini (hawamo pichani) wakati akifungua mkutano wa tathmini wa awamu ya kwanza ya utaratibu wa Maafisa Mawasiliano kuzungumza na waandishi wa habari, ambapo aliwataka kutekeleza utaratibu huu kama ulivyopangwa ili kuweza kutoa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Sera na Miradi inayoratibiwa na Ofisi zao kwa wananchi kupitia waandishi wa habari, katika mkutano uliofanyika jana Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
MKURUGENZI wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali Assah Mwambene akiongea na Maafisa Mawasilino Serikalini (hawamo pichani) jana wakati mkutano wa tathmini wa awamu ya kwanza ya utaratibu wa maafisa mawasiliano kuzungumza na waandishi wa habari, ambapo alisisitiza utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Sera na Mipango pamoja na kujibu hoja mbalimbali zinazohusu Ofisi zao. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
MKURUGENZI Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa Akiwasilisha ripoti ya utekelezaji Mikutano ya awamu ya kwanza ya utaratibu wa maafisa mawasiliano kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu Sera na Mipango pamoja na ujibuji wa hoja mbalimbali zinazohusu Ofisi zao, kwenye katika mkutano uliofanyika jana Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Innocent Mungy akiwasilisha kwa Maafisa Mawasilino Serikalini juu ya namna bora ya kuandaa na kuboresha taarifa kwa vyombo vya habari, katika mkutano uliofanyika jana Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa Mawasilino Serikalini waliohudhuria mkutano huo wa tathmini uliofanyika jana katika Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA HASSAN SILAYO-MAELEZO).