Tabitha Leah Ritchie
Na. Mo Blog Team
MWANAMKE mmoja mkazi wa Toronto, Canada amekamatwa katika uwanja wa ndege wa Bogota, Colombia akijaribu kusafirisha kilo mbili za madawa ya kulevya aina ya cocaine kwa kujifanya mja mzito.
Kanali Esteban Arias amesema kwamba mwanamke huyo mwenye miaka 28, Tabitha Leah Ritchie alisimamishwa wakati akijaribu kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Canada baada ya mkaguzi mmoja kubaini kwamba tumbo lake lilikuwa gumu sana na lenye ubaridi hali isiyo ya kawaida.
Amesema kwamba polisi waligundua tumbo la bandia likiwa limefungwa kwenye mwili huku ndani kukiwa na kilo mbili za cocaine.