Na. HAMAD SHAPANDU, Pemba
Mimba katika umri mdogo zimeelezwa kuleta athari kubwa huko wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba nakusababisha maisha magumu kwa wanawake na familia zao pamoja na kukosa wataalamu wa ushauri wa Afya ya uzazi toka katika taasisi mbalimbali.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Dakta Rashid Daudi Mkasha akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi amesema kwamba moja ya athari kubwa ya mimba katika umri mdogo nikushindwa kwa wanawake hao kutumia huduma za kliniki ipasavyo jambo ambalo linapoteza nguvu na uwezo kujua mwenendo mzima wa afya ya mama na mtoto.
Uwezo mdogo wa kujifungua kwa wanawake hao imekuwa kikwazo kikubwa kinachosababisha wanawake kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua,kukosa ushauri nasaha,bali viungo vya wanawake hao havijakomaa kuhimili vishindo vikubwa vya kuijfungua ,na kuharibika kwa sehemu za ndani kutokana na kukosa ushauri bora wa kitaalamu hali inayoweza kusababisha vifo visivyotarajiwa Dakta, Rashid alisema.
Ingawa Dakta, Rashid hakueleza bayana takwimu za wanawake wanaokumbwa na mikasa hio huko wilaya ya Micheweni hali sio ya kuridhisha kutokana na dharau ya baadhi ya watu kupuuza ushauri wanaopewa wa kitaalamu kwa wanandoa na ugumu zaidi upo kwa wanawake wanaobeba mimba wakiwa shuleni.
‘wari na wajane ambao wanakuwa na siri kubwa yakuogopa watu wasiijuwe siri yao mapema nakuchelewa kwenda kliniki na hata wakati wakujifungua wakipata tabu hucheleweshwa kwenda kliniki kwa wakati mpaka waone hali ni mbaya zaidi,” amesema.
Afisa Elimu na Mafunzo ya Amali wa wilaya ya Micheweni Mbwana Shaame Saidi amesema kuwa mimba katika umri mdogo zimeathiri sana sekta ya elimu wilayani humo kwa kuwaacha wanawake wengi wakisalia kidato cha pili na wakishajifungua wengi wao wanaona aibu na kushindwa kurejea shuleni.
Ukiacha ndoa zisizotarajiwa wilaya ya Micheweni imepata kipigo kikubwa cha kukosa wataalamu katika sekta mbalimbali za jamii kukosa wataalamu wanawake hasa katika sekta ya afya ambayo wanawake wamekuwa wakidai wazalishwe na wanawake wenzao lakini wapi hawapo wakuwahudumia kwa kukosa elimu afisa huyo alisema.
Amefahamisha kuwa kutokana na takwimu zilizopita wilaya ya michewni idadi ya wanawake waliohitimu elimu ya juu (degree) ni thalathini tu hali ambayo inatia ufukara wa kukuza utendaji wao nakuwa juhudi zaidi inahitajika kwa wazazi kuacha tabia ya kuona ukimuoza mume mwanafunzi wa shule umeitia hasara na umaskini familia hio.
Amebainisha kuwa baadhi ya wazazi wanapoona wizara ya elimu wamegundua siri ya kuwepo kwa ndoa baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwasafirisha watoto wao hadi Unguja au Dar es salaam kuwafungisha ndoa na kuwa ujanja huo unazidhalilisha familia hizo ingawa wenyewe hawajui.
Baadhi ya wazazi waliozungumza na Mwandishi wa Habari wamesema kuwa ugumu wa maisha ndio uliochangia hali hio kwa kuwa mwanafuzi akimaliza kidato cha pili gharama za kumpeleka mwananfuzi aendelee na masomo ni ngumu huku wengi wao wakidai wanaishi chini ya dola moja kwa siku hawezi kuongeza mzigo zaidi huku usemi wakuwa akiwa tayari mpeleke ukizidisha umaskini kwa baadhi ya familia.