Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Bodi yaanzisha kiapo kwa wahandisi wataalamu

$
0
0

4- magufuli (kulia) akizindia kiapo(kati hakimu na (shoto) msajili steven

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akizindua rasmi kiapo cha utii kwa Wahandisi Wataalamu jijini Dar es Salaam kilichofanyika katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wahandisi 2013. Picha kushoto ni Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini Mhandisi Steven Mlote, (katikati) ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Wariyaruandwe Lema.

7- wazri magufili (kulia)akimkabidhi mwanafunzi bora wa kike  Anna Msingwa

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akimkabidhi cheti pamoja na laptop Anna Msigwa mmoja ya mhandisi mhitimu aliefanya vizuri zaidi katika mtihani wa mwisho wa mwaka 2012/ 2013, (Pichani mwenye kipaza sauti) Ni Msajili wa Bodi ya Wasajili Mhandisis Steven Mlote.

8-Nora abdalla(kush) akikabidhiwa cheti na Magufuli (kulia)

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akimpatia cheti Mhandisi mhitimu Nora Abdalla kati ya aliefanya vizuri zaidi katika mitimani yao ya mwaka wa mwisho2012/2013. (katikati)Masjili wa Bodi ya Wahandisi Mhandisi Steven Mlote.

5 mama hakimu akiwaapisha makandarasi(kulia)

 

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Wariyaruandwe Lema(kulia) akiwaapisha Wahandisi mbalimbali kutoka taasisi na mashirika ya kihandisi jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya wahandisi 2013  jijini Dar es Salaam.

6-baadhi-ya-wahandisi-wakila-kiapo

Baadhi ya wahandisi wakila kiapo cha utii jijini Dar es Salaam.

9- baadhi ya wanafunzi bora wakifuatiaa hotuba ya waziri

Baadhi ya Wahandisi waliohudhuria hafla ya maadhimisho ya siku ya Wahandisi 2013  jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (hayupo pichani.)Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

3- washi

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Wahandisi wataalamu (Professional Engineers) wapatao 50 wamewaapishwa na Bodi yao kiapo cha utii kwa taaluma yao na wameahidi kwamba itakuwa mwiko kwao kukiuka miiko ya taaluma ya uhandisi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alipokuwa akizindua kiapo cha wahandisi wataalamu (Professional Oth) jijini Dar es Salaam katika siku ya wahandisi mwaka huu ili kuhakikisha kuwa wanawajibika vyema kwenye taalum, kuwajibika katika maamuzi na utekelezaji wao wa kila siku.

“Nimefurahishwa sana na bodi yenu kwa kitendo cha kuwaapisha wahandisi, kuwepo kwa kipengele cha kumwogopa Mungu kitatusaidia sana ili tuwe hata na huruma na tuwasaidie watanzania” alisema Magufuli.

Lengo kuu la kiapo ni kuwakumbusha wahandisi majukumu yao ya kitaaluma na umuhimu wa kuzingatia taaaluma wakati wote na kuufanya umma ujenge imani kwa wahusika.

Aidha kiapo kitatumika dhidi ya mhandisi atakapovunja miiko ya taaluma katika utendaji wake wa kazi ambapo vyombo mbalimbali vya kisheria vitatumia kiapo hicho kumchukulia hatua atakayekiuka kiapo chake. 

Kwa upande wake hakimu aliyewaapisha wahandisi hao kutoka Mahakama ya Kisutu Warialanga Lema aliwaasa kuwa wakumbuke kiapo walichokula, kwa kwa kufanya hivyo kutawawezesha kuzingatia maadili ya kazi zao za kila siku na kuitendea haki taaluma hiyo na mwishwe kuwa waaminifu kwa nchi yao.

Wahandisi waliokula kiapo wlikabidhiwa leseni ya uhandisi, nakala ya kiapo pamoja na maadili na miiko ya kihandisi. Zana hizi zitatumika wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kuhandisi wakati wanazitumikia taasisi zao na taifa kwa ujumla ili liweze kufikia malengo ya millenia kwa kutumia utaalamu wao.  

Naye mwenyekiti wa bodi hiyo Mhandisi Prof Ninatubu Lema alisema kuwa siku ya wahandisi inamaana kubwa kwao malengo yake ni pamoja na kuiwezesha jumuiya ya wahandisi kuuonesha umma nini wahandisi wa Tanzania wanaweza katika kuleta maendeleo ya nchi.

Uzinduzi huo uliambatana na tuzo zolizotolewa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi ili kuwafanya vijana washawishike kusomea taaluma ya uhandisi. 

“Nia yetu katika siku hii ni kuatia moyo wanafunzi wa kitanzania wasome uhandisi ili mwafanye vizuri zaidi katika masomo yao” alisema prof. Lema.

 Prof. Lema aliwataja  wanachuo walifanya vizuri katika masomo yao kwa kupata alama zenye GPA ya 4.0.

Baadhi ya wanafunzi hao ni pamoja na Anna Msigwa, Dnaiel Mkama, Hamfrey Swai, Menradi  Kilemile, Godifrey Gabriel, Godfrey Elias, liliani Kamala, Nyarobi Kasanda, Jean Mdula, Said Sudi, Norah Abdalah, Laila Ngude, Sophia Nahodha, Astarina Kilindi, Solomoni Komba, Athon Richard na Silasi D. Silas

Wahitimu hawa wamefanya vizuri katika masomo yao kutokana na tabia zao nzuri inayobainishwa na haiba waliyonayo, kwani miongoni mwa hawa hakuna aliye na mavazi yaliyovaliwa “nusu mlingoti” (mlegezo).

Siku ya wahandisi mwaka huu imepambwa kwa ushiriki wa takribani wahandisi wapatao zaidi ya 1000 kutoka taasisis mbalimbali ambazo ni Chuo cha Uhandisi na Teknolojia cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CoET), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Chuo cha Uhandisi na Teknolojia cha St. Joseph (SCET), Chuo cha Aridhi (ARU), Makandarasi mbalimbali, Makampuni za Ushauri wa Kihanndisi, mashirika na Makampuni ya Kibiashara na Taasisi za Utafiti.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles