Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Mama Kikwete atunukiwa tuzo ya kimataifa ya jitihada za kuendeleza rasilimali watu katika taifa kwa mwaka 2012.

$
0
0

3edfMama-Salma-Kikwete

Mwenyekiti wa WAMA Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

Na Anna Nkinda – Maelezo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya kimataifa ya jitihada za kuendeleza rasilimali watu katika taifa kwa mwaka 2012 na Taasisi ya Bright Entertainment Network (BEN) ya nchini Uingereza.

Tuzo hizo pamoja na cheti amekabidhiwa leo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) zilizopo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Dkt. Mukangara alikabidhiwa tuzo hiyo na Taasisi ya BEN mwezi wa sita mwaka huu alipokuwa nchini Uingereza kwa shughuli za kikazi ili aifikishe kwa  Mama Kikwete.

Dkt. Mukangara  amesema kuwa tuzo hiyo ambayo inafahamika kwa jina la “Country Human Development – 2012 Award” inatolewa kwa mshindi anayeteuliwa na Taasisi ya BEN ikiwa ni miongoni mwa waliowania kutoka nchi za Bara la Afrika , Carribbia, Asia na Pasifiki.

Waziri Dkt. Mukangara amesema “Ushindi huu wa kimataifa Mama Kikwete umeupata kutokana na juhudi na harakati zako za kuwainua kimaendeleo wananchi wa matabaka mbalimbali hapa nchini, hasa wasichana na kina mama kupitia Taasisi uliyoiasisi na kuendelea kuiendesha ya WAMA.

Sote tunakubalina kutokana na kazi tunazozishuhudia ambazo Taasisi yako chini ya uongozi wako inazifanya, hakika umestahili kutunukiwa tuzo hii ya jitihada za kuendeleza rasilimali watu katika taifa hongera sana”.

Kwa upande wake Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa WAMA amemshukuru Waziri Dkt. Mukangara kwa kuchukua dhamana ya kupokea tuzo hiyo na kuifikisha kwake, pia aliishukuru Taasisi ya BEN kwa kuona umuhimu wa kazi anazozifanya na kumchagua kuwa mmoja wa washindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2012, kwani watu walioshiriki ni wengi kutoka ndani na nje ya bara la Afrika.

Mama Kikwete amesema “Ninashukuru sana kwa tuzo hii niliyoipata ambayo inazidi kunipa moyo na ninaahidi nitaendelea kufanya kazi kwa kujituma kadri Mwenyezi Mungu atakavyo niwezesha na sintarudi nyuma kuwasaidia watanzania, eti kwa kuwa nimepata tuzo kwani sikutegemea kuwa ipo siku nitapata tuzo kutokana na kazi ninazozifanya za kuisaidia jamii”.

Hii tuzo ni kwa ajili ya  watanzania wote na wafanyakazi wa taasisi ya WAMA, kwani bila ya watanzania nisingeweza kupata tuzo kama hii”.

Mwenyekiti huyo wa WAMA amesema taasisi zote za maendeleo zitaendelea kufanya kazi kwa bidii ili ziweze kutimiza malengo ya Maendeleo ya Milenia kwa wakati uliokusudiwa.

Kazi zinazofanywa na Taasisi ya WAMA zilizopelekea Mwenyekiti wa Taasisi hiyo kupewa tuzo ni uraghibishi wa kuboresha, hali ya maisha kwa watoto, wasichana na wanawake hasa kwa upande wa afya, elimu na uchumi na kuwasaidia mitaji kinamama wajasiriamali.

Zingine ni kupambana na mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari  na kuendesha  mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa kina mama, hususani kupunguza maambukiziya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

 

 

 

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles