Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali mwenyekiti wa UDP Mh.John Momose Cheyo aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.Katikati ya Rais na Mama Salma ni Mjukuu wa Mheshimiwa Cheyo anayejulikana kama Gabriel Cheyo. (Picha Freddy Maro).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa leo, Jumanne, Agosti 6, 2013, amemtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Bariadi Mashariki, Mheshimiwa John Momose Cheyo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, mjini Dar Es Salaam.
Rais Kikwete ambaye amezungumza kwa muda na Mheshimiwa Cheyo amempa pole na kumtakia apone haraka na ili aweze kuendelea na shughuli zake za uwakilishi wa wananchi wa Bariadi Mashariki.
Mheshimiwa Cheyo amelezwa Aga Khan tokea asubuhi ya juzi, Jumapili, Agosti 4, 2013.