Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Benki ya Dunia yaipa changamoto Afrika kuboresha matumizi ya ardhi kuondoa umasikini.

$
0
0

Makhtar Diop

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika Makhtar Diop.

Benki ya  Dunia imetoa changamoto kwa nchi za Afrika  kuhimiza maendeleo endelevu ya  ardhi  ili kupunguza umaskini na kujiletea maendeleo.

Ripoti ya Benki hiyo imeeleza kuwa ingawa nchi za Afrika zina karibu nusu ya eneo la ardhi nzuri  ambayo haijaendelezwa kwa kilimo, bara hilo limeshindwa  kuiendeleza ardhi hiyo inayokadiriwa kuwa hekta milioni  202 kujikwamua katika umaskini, kuleta maendeleo ya uchumi, kuongeza nafasi za kazi na kuleta mafanikio kwa jumla.

Ripoti hiyo inayoitwa  “Kutumia ardhi ya Afrika kwa mafanikio ya pamoja,”  inaeleza kuwa  nchi za Afrika na jamii zake zinaweza kabisa kuondoa tatizo la uporaji wa ardhi, kuzalisha mazao ya chakula na kubadilisha  taratibu za usimamizi na umiliki wa ardhi katika mwongo ujao.

Ripoti  hiyo imeeleza, Afrika ina kiwango kikukbwa cha umaskini ambapo asilimia  47.5 ya watu wake wana kipato chini ya  dola 1 za Marekani ($1.25)kwa siku.

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika Makhtar Diop amesema licha ya kuwa na ardhi kubwa na utajiri wa madini, Afrika bado ni maskini.

Ameongeza kuwa kuboresha usimamiaji wa ardhi ni muhimu kwa maendeleo ya haraka na kutoa nafasi  zaidi kwa waafrika, wakiwemo wanawake ambao ni asilimia 70 ya wakulima wa Afrika, ambao wanakwazwa  kumiliki ardhi na sheria za kimila na kuwa hali hii haikubaliki na lazima ibadilike ili waafrika waweze kunufaika na ardhi yao.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia.

Hata hivyo kumekuwa na matumaini ya maboresho  chini ya mipango inayoendelezwa katika nchi za   Ghana, Malawi, Msumbiji,, Tanzania, na Uganda, ambapo  mpango wa kutumia  ardhi kwa mafanikio ya pamoja  unaweza kuleta mapinduzi  ya  uzalishaji wa kilimo na uporaji wa ardhi na  kuondoa umaskini wa kutupa barani Afrika.

Ripoti hiyo inapendekeza kuwa Afrika inaweza kufanikiwa kuendeleza ardhi yake katika kipindi cha muongo ujao kwa na mabadiliko  na uwekezaji, kurasimisha ardhi  na  maeneo muhimu yanayomilikiwa na watu binafsi. 

Pia kusimamia taratibu za umiliki za maeneo yaliyovamiwa  na kujengwa  bila mpangilio mijini ambapo wanaishi zaidi ya  watu asilimila 60 barani Afrika na kukabiliana na udhaifu wa utawala na rushwa katika mfumo wa  usimamizi wa ardhi katika nchi za Afrika ambao, kwa kawaida unapendelea wakubwa na kuathiri maslahi ya wananchi walio maskini.

Akifafanua zaidi Makhtar Diop amesema Serikali za Afrika zinatakiwa kuwa na dhamira  ya kisiasa kuhimiza  mabadiliko haya ya ardhi kuvutia raslimali na uwezekezaji wa jamii ya kimataifa. .

Ripoti  hiyo inasema kuwa mpango huo utagharimu  nchi za Afrika  na  washirika wa maendeleo , ikiwemo sekta bianfsi kiasi cha  dola za Marekani bilioni 4.5  katika kipindi cha miaka 10 kuleta mabadiliko ya sera na uwekezaji.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles