Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, aliyefariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Makamu alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini jana Julai 19, 2013. (Picha na OMR).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa ndugu wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo, nyumbani kwa marehemu, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya waombolezaji katika msiba wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhani na kuaga msiba huo.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu katika msiba huo leo.