Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Rais Dkt. Shein amteua Said Bakari kuwa Mwenyekiti wa SUZA.

$
0
0

Dr-Ali-Mohamed-Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein  (Pichani) amemteua Said Bakari  Jecha  kuwa Mwenyeki wa Baraza la  Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).

Dkt Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 9(1)cha Sheria ya chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Namba 8 ya mwaka 1999

 Aidha Dkt Shein amemteua Abdulrahman Rashid kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB)

Dkt Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu  wa  uwezo  alipewa chini ya kifungu  Namba  8 (a) (1) cha  sheria  ya  Bodi  ya  Mapato  Zaznzibar (ZRB)  Namba 7 ya mwaka 1996 kama  ilivyorekebishwa  na Sheria Namba 8 ya 2009.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi  Dkt.Abdulhamid  Yahya Mzee ,Uteuzi wa Said Bakar Jecha unaanzaa  Julai 20,na uteuzi wa Abdulrahman Rashid  unaaza Julai 18 mwaka huu.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles