Ndoa za watu wa jinsia moja zitahalalaishwa katika mataifa ya England na Wales, baada ya bunge la Uingereza kuidhinisha mabadiliko ya mwisho katika sheria ambayo inaungwa mkono na Waziri Mkuu David Cameron.
Sheria hiyo imesababisha mgawanyiko katika chama cha kihafidhina (Conservative) cha David Cameron.
Sheria hiyo inaungwa mkono na vyama vingine wiwili vikubwa nchini Uingereza vya Labour na Liberal Democrats.
Wabunge wa chama cha Conservative wamepiga kura mara mbili kuipinga sheria hiyo.
Mswada wa sheria hiyo ulipitishwa baada ya mdahalo uliodumu kwa saa mbili na inasubiri kutiwa saini na Malkia Elizabeth kuwa sheria.