Wanaharakati nchini Nigeria wamefungua kesi katika mahakama kuu ya shirikisho mjini Abuja, wakitaka kukamatwa kwa rais Omar al-Bashir wa Sudan ambaye amewasili nchini humo, kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika kuhusu Ukimwi.
Al- Bashir amewekewa waranti wa kukamatwa na mahakama ya kimataifa ya Uhalifu-ICC yenye makao yake mjini the Hague, Uholanzi.
Rais huyo anashutumiwa kupanga mauaji ya kuangamiza na makosa mengine katika ghasia zilizouwa watu takriban 200,000 katika jimbo la Darfur.