Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Uratibu Dhaifu Utaua Misitu ya Afrika Mashariki.

$
0
0

forest_semuliki

WADAU wa masuala ya misitu katika ukanda wa Afrika Mashariki wameziomba serikali za nchi hizo kuongeza nguvu katika uratibu wa biashara ya mbao ili kuokoa misitu na viumbe vyake visitoweke kwenye eneo hilo.

Katika taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari iliyotolewa jijini mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku mbili wa wadau wa misitu uliofanyika Dar es Salaam, washiriki walisema kwa ufuatiliaji uliopo sasa, mustakabali wa misitu na wanyamapori uko hatarini.

 “Biashara ya mbao na mazao mengine ya misitu imeongezeka sana baina ya nchi hizi katika miaka ya karibuni. Ni kweli kwamba bado sehemu kubwa inasafirishwa kwenda Asia na Ulaya lakini biashara baina ya nchi zetu ni kubwa na ndiyo maana ni muhimu kuweka mikakati ya pamoja kudhibiti biashara hii,”  ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Mkutano huo ulikuwa na washiriki kutoka katika nchi za Tanzania, Kenya na Msumbiji na uliitishwa kwa lengo la kutathmini biashara isiyo halali na endelevu ya mbao katika nchi za Afrika Mashariki.

Mkutano huo uliandaliwa na kufadhiliwa na Mfuko wa Kimataifa wa Wanyamapori na Maliasili (WWF) kupitia mpango wake wa TRAFFIC na Jukwaa la Maliasili la Tanzania (TNRF).

Katika mkutano huo, ilielezwa kwamba Kenya kwa sasa imeibuka kuwa kinara wa kupokea mbao na bidhaa nyingine za misitu kutoka katika nchi nyingine za Afrika Mashariki, ingawa haijabainika iwapo vinatumika Kenya kwenyewe au nchi hiyo inatumika kama njia ya kusafirisha vitu hivyo kwenda Asia na Ulaya.

Kutokana na kutoka kwa taarifa hiyo, wadau walipendekeza kwamba serikali za Tanzania na Kenya zinapaswa sasa kuingia katika makubaliano maalumu ya kulinda maliasili hizi (MoU) kama ilivyo kwa nchi za Tanzania na Msumbiji zilizoingia makubaliano kama hayo Aprili mwaka jana.

 “Tunapendekeza kwamba mchakato wa kuandaa MoU hiyo uanze haraka iwezekanavyo ili utekelezaji wake uanze bila ya kuchelewa. Bila ya makubaliano ya namna hii, misitu yetu itakuwa katika hatari ya kweli kabisa kutoweka,” walisema washiriki wa mkutano huo.

Mkutano huo wa wadau uliweka wazi mapungufu yaliyopo katika suala zima la utawala wa udhibiti wa biashara ya mbao Afrika Mashariki ikiwamo kutokuwapo kwa taarifa kuhusu kiwango kinachovunwa na kuuzwa nje, ulinzi mbovu wa rasilimali zenyewe, upungufu wa watumishi na uwepo wa sera zinazotofautina kwa nchi tofauti katika masuala hayo.

Mratibu wa TRAFFIC kwa ukanda wa Afrika Mashariki, Julie Thomson, alisema mkutano huo uliitishwa kwa lengo la kuangalia hali ilivyo sasa mara baada ya kutoka kwa ripoti ya TRAFFIC ya mwaka 2007 –Iliyotoa taarifa nyingi kuhusu biashara hiyo haramu ya mbao na mazao ya misitu, na pia kuangalia nini kinahitajika kufanyika kwa sasa.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles