Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Kampuni ya Steps Entertainment yanogesha Tuzo za Bongo Movie.

$
0
0

IMG_4506

 Pazia la Tuzo za Steps Bongo Movie Awards 2012-2013 lilizinduliwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa.

IMG_4726

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akimkabizi tuzo ya mwongozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 Vicent Kigosi ‘Ray ‘ wakati wa utoaji wa tuzo hizo na kushudiwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza Steps Entertainment  inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.

IMG_4735

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akifafanua jambo baada ya kumkabizi tuzo Vicent Kigosi ‘Ray’ ya mwogozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 wakati wa utoaji wa tuzo hizo.

IMG_4559

Mzee Majuto akipokea Tuzo ya msanii bora wa uchekeshaji.

IMG_4576

Msanii Steve Nyerere akipokea Tuzo.

IMG_4609

Msanii Nice Mohamedi ‘Mtunis’ akipokea tuzo ya Mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Steps Entatainment tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.(Picha nawww.burudan.blogspot.com).

IMG_4710

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps, Diresh Solanki akimpa tuzo msanii bora wa kiume katika tasnia ya filamu nchini Jacob Steven JB wakati wa utoaji wa tuzo hizo na kushudiwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.

297507_539116066134541_657693458_n

Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandaliwa na kampuni ya Steps Entertainment.

IMG_4634

Msanii Shilole akiwa jukwaani.

IMG_4685

Mpiga Picha Mohamed Aralakia  za kava Mbalimbali za Kampuni ya Steps akipokea Tuzo.

IMG_4760

Baadhi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabiziwa tuzo zao za kwanza kwa mwaka 2012 zilizoandaliwa na kampuni ya Steps Entertainment.

Kampuni  ya Usambazaji wa filamu ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo.

Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo.

Baadhi ya washindi ambao walipatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Steven Mangendela ‘Steve Nyerere’, Issa Mussa ‘Cloud 112′ Mohamed Nurdini ‘Chek budi’ Nice Mohamed ‘Mtunisi’ Iren Paul akinyakuwa msanii bora chipkizi wa kike

Wakati katika kinyang’anyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Steven ‘JB’ huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Iren Uwoya

na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda ‘Jimmy Masta’

Wakati katika kipengere cha muhongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi’ Ray’ na kampuni yake ya RJ Filamu

mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri rakini kwa sasa awapo duniani moja ni kwa Stevin Kanumba,Saidi Kilowoko ‘Sajuki’ John Stefano,Hussein Ramadhani Mkiety,’Sharo Milionea’

Katika utoaji wa tuzo huzo kulikua na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles