Mwana FA akiwasili katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam huku akiwa amevalia suti matata iliyotengenezwa na mbunifu wa mavazi anayekuja kwa kasi nchini Sheria Ngowi.(Picha zote na Geofrey Mwakibete wa Mo Blog).
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA akikamua jukwaani wakati wa Show ya Kijanja ya The Finest iliyorindima usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar. Nyuma yake ni Msanii Linah aliyeshirikishwa kwenye nyimbo ya YALAITI aliyoimba na Mwana FA akisubiri kutumbuiza.
Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini Ben Paul akisindikiza kutoa burudani wakati wa show ya Mwana FA iliyopewa jina la “The Finest”. Wasanii wote walionekana nadhifu kwa kuvaa masuti ya gharama.
Kutoka (kulia) ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe, akiwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba, wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wa Mwana FA, waliohudhulia shoo hiyo. Kushoto ni Mtangazaji wa Clouds FM, Gerald Hando.
Mashabiki wa Mwana FA, wakimshangilia Superstar wao wakati akitoa burudani.
Mrembo wa Wema Sepetu na Kidate wake nao walikuwepo kwenye show ya wajanja.
Mashabi wa Mwana FA wakionekana kukongwa mioyo yao wakati wa show iliyobeba jina la “THE FINEST”…Na kweli ilikuwa The Finest kama inavyoonekana pichani.
Watu weweeeeeeeeeee…..ukumbi ulirindima Shangwe za mashabiki wa Mwana FA.
Mwana FA akiendelea kuwapa raha mashabiki wake.
Wadau wakishow love nje ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.