CHAMA CHA MAPINDUZI – TAWI LA UINGEREZA – UNITED KINGDOM
Website ccmuk.org, Blog ccmuk.org/blog, Facebook page chama cha mapinduzi uingereza, twitter CCMUK 1
Contacts Phone +44 74 04 863333, +44 7545 213515
E-mail – itikadi-uenezi@ccmuk.org
Aidha CCM UK inayo imani kubwa kuwa Sherehe hii ya Pasaka itakuwa kigezo cha kuwakaribisha Watanzania wa Imani zote kujitazama kwa wongufu na kuridhia misingi mikuu ya Uhuru, Muungano wetu na Umoja wa Taifa letu.
CCM UK inaungana na Watanzania wote kukememea dhidi ya vichocheo vya aina zote vinavyohatarisha umoja wa TAIFA LETU, usalama wa raia na mali zao, uhuru wao wa kuabudu na kusujudu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Kwa kuwa Dhamira kuu ya Pasaka ni kujenga Upendo, Mshikamano, Umoja na Uhuru, hasa katika kipindi hiki cha kutafakari mchakato wa Kupata KATIBA MPYA yenye kukidhi kiu ya maendeleo kwa Wananchi Kiuchumi na kimaendeleo kama Taifa moja, CCM UK inawatakia kila la kheri katika kusheherekea sikukuu hii muhimu kwa Wakristo wote Duniani kwa Amani na Utulivu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Imetolewa na Abraham Sangiwa - Idara ya Siasa na Uenezi.
CCM – TAWI LA UINGEREZA – UNITED KINGDOM.
20th April -2014