Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Rais Kikwete awasili Brussels kuhudhuria kikao cha wakuu wa nchi wa nchi za Afrika na za Umoja wa Ulaya (EU-Africa Summit)

$
0
0

Jakaya-Kikwete1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Brussels,  Ubelgiji leo asubuhi 2 Aprili,2014 kuhudhuria kikao cha siku mbili cha Wakuu wa Nchi wa nchi za Afrika na za Umoja wa Ulaya (EU-Africa Summit).

Kikao  hiki cha siku 2 kitatoa nafasi kwa viongozi hawa kutathmini mafanikio ya uhusiano wao  na  kutafuta njia zingine mpya za kuboresha mahusiano hayo .

Kauli mbiu ya mkutano wa Mwaka huu inasisitiza katika kuwekeza kwa watu,Mafanikio na Amani (Investing in people, prosperity and peace) na baadaye kufanya mazungumzo na  Rais wa Kamisheni wa Nchi  za Ulaya (EU) Bw. Jose Manuel Barosso.

Akiwa Brussels Rais Kikwete anatarajia kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki  Moon na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mheshimiwa Mark Rutte.

Rais Kikwete anatarajia kuondoka Brussels mara baada ya Mkutano kumalizika na kurejea Dar es Salaam.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles