Rais Jakaya Kikwete akikabidhi kombe kwa mshindi wa pili wa tuzo wa mzalishaji bora wa mwaka 2013, kwa Mkurugenzi wa Huduma ya Makampuni na Masuala ya Sheria wa kampuni ya Bia ya TBL, Stephen Kilindo wakati wa hafla ya makabidhiano ya tuzo hizo yalifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia) wakati wa kushoto ni Mwenyekiti Mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP ambayo ilikuwa mdhamini mkuu wa hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akipiga picha na Watendaji Wakuu wa kampuni ya Bia TBL mara baada ya kuwakanidhi tuzo ya mzalishaji bora wa mwaka 2013 inayotolewa na CTI.
Watendaji wakuu wa TBL wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mzalishaji bora wa mwaka 2013 inayotolewa na CTI.