Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Wakazi wa Dodoma waja na maoni tofauti juu ya muungano

Image may be NSFW.
Clik here to view.
warioba pics

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Na Damas Makangale, MOblog aliyekuwa Dodoma

Baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuwasilisha Rasimu ya katiba mjini Dodoma hivi karibuni wakazi wa mji huu mkuu nchini wamekuwa na maoni tofauti kama walivyozungumza na MOblog Tanzania.

Wakazi hao ambao wengi wao ni kutoka katika maeneo ya area d, c, chamwino na vitongoji vingine vya mji wa Dodoma wamempongeza kwa namna mbalimbali Jaji Warioba kwa kuwa ukweli na hali halisi ya Muungano kati ya bara na visiwani.

Akizungumza na MOblog hivi karibuni jijini Dodoma, Alfa Musa amesema kwamba mzee warioba ameeleza ukweli kwamba kwa hali iliyoko sasa hatuwezi kuendelea kuwa na serikali mbili na nchi mbili kwa sababu aina hiyo muungano utapelekea kuwepo na malalamiko zaidi mbele ya safari.

“pamoja na kwamba wajumbe wengi wa katiba walimshangilia sana katika maeneo mengi bado sisi wananchi tuna wasiwasi na msimamo wa CCM kwa kuendelea kuwa na imani na muundo wa serikali mbili,” amesema Musa Mkazi wa Mazimbu Iringa road.

Musa alilisitiza kwamba matatizo ya Muungano kati ya bara na visiwani yalianza tangu enzi za Aboud Jumbe Mwinyi mwaka 1984 kwa kile kilichoitwa kuchafuka kwa hali ya hewa na kila mtanzania anajua kilichotokea kipindi kile.

Amesema kwamba Aboud Jumbe Mwinyi alitaka kubadili katiba na akilalamika kwamba serikali ya Tanganyika imejificha kwenye koti ya muungano na kuua taifa la Zanzibar kama nchi kamili.

Kwa upande, Mary Emmauel amesema kwamba Jaji warioba anapendekeza serikali tatu kwa maana kuwe na marais wa tatu kwenye nchi mbili kwa kweli hii ni matatizo na mzigo kwa walipa kodi wa Tanzania.

‘mimi napenda kuungana na msimamo wa chama tawala kwa muundo thabiti kabisa wa kudumisha muungano wetu ni serikali mbili na wala si tatu kwa sababu kutaleta mshikamano na utengamano zaidi wa watu wa nchi hizi mbili,’ amesema merry

Amesema kwamba hata waasisi wa nchi mbili walikuwa wanatamani kuwe na serikali hata moja na nchi moja katika kudumisha udugu wa enzi na enzi kati ya watanganyika na wazanzibari.

Emmanuel aliongeza kwamba hakuna muungano wowote hata wabiashara ambao ukakosa kasoro au changamoto kwa hiyo matatizo ya muungano bado yanaweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

“tunajua kwamba kuna baadhi ya wazanzibar na watanganyika wanalalamika kuhusu mambo mbalimbali kama vile utaifa, ardhi, gesi na vitu vingine lakini hivi vyote vinaweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa viongozi na wananchi kukaa meza moja ya majadiliano,” amesema

Mfanyabiashara Hassan Mohammed yeye anasema kwamba muungano wa Tanganyika na Zanzibar unatakiwa uwe wa mkataba tu kwamba baada ya muda unaweza kuvunja na pande yoyote endapo unaona unawabana katika maeneo nyeti kwa maslahi ya upande husika.

“hata karume alisema kwamba muungano kama koti ukiona linakubana unaweza kulivua tu kwa kuzingati hali halisi ya mambo yanavyokwenda,” amesema Mohammed 

Katika hotuba yake ya maneno 14,112 iliyosomwa kwa saa 3:34, Jaji Warioba aliweka wazi maoni ya wananchi yaliyomo katika ibara 271 za Rasimu hiyo, ukiwamo muundo wa Muungano wa Serikali Tatu – Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.

Mwanasheria huyo alijenga hoja zake zilizoisaidia Tume yake kufikia hitimisho la muundo huo, kwamba ilizingatia maoni ya wananchi, yakiwamo ya mabaraza ya katiba ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambayo ama moja kwa moja au kwa tafsiri yalipendekeza muundo wa Serikali Tatu.

Amesema tume hiyo ililazimika kupendekeza muundo huo kutokana na kero, hoja na malalamiko yaliyotolewa na pande mbili za Muungano wakati tume hiyo ikukusanya maoni, pamoja na hoja zilizotolewa miaka ya nyuma na tume mbalimbali.

“Suala la muundo wa Serikali Tatu limechukua nafasi kubwa katika mjadala tangu tume ilipozindua Rasimu ya Kwanza ya Katiba. Mjadala wa muundo wa muungano umekuwa mkubwa kiasi cha kufunika mapendekezo mengine yaliyomo katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano,” amesema Warioba

Huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe, Jaji Warioba amesema kwa tahmini ya tume hiyo, muundo wa Serikali mbili hauwezi kubaki kwa hali ya sasa.

“Muungano wa Serikali mbili waliotuachia waasisi siyo uliopo sasa. Umebadilishwa mara nyingi, wakati mwingine bila ya kufanya mabadiliko kwenye Katiba.  Waasisi walituachia Muungano wa nchi moja yenye Serikali mbili na siyo nchi mbili zenye Serikali mbili,” amesema.

Amesema muundo wa Serikali mbili unaweza kubaki tu ikiwa orodha ya mambo ya muungano haitapunguzwa bali itaongezwa na isipokuwa hivyo Serikali ya Muungano itabaki na rasilimali na mambo ya Tanzania Bara tu.

“Katika hali hiyo, pande zote mbili zitaendelea kulalamika. Kwa upande mmoja, Zanzibar itaendelea kulalamika kwamba Tanzania Bara imevaa koti la Muungano kwa faida yake na kwa upande mwingine, Tanzania Bara itaendelea kulalamika kwamba mambo yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara na rasilimali zake, ndizo zimekuwa Muungano,” amesema. 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles