Ajali imehusisha gari ya abiria aina ya hiace inayofanya safari zake kati ya Mweka na Moshi mjini na Landcruiser VX iliyokuwa imewabeba wanafunzi wa chuo cha usimamizi na uhifadhi wa wanyama pori Mweka kilichopo Mweka , Moshi vijijini.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo bwana Fred Mushi amesema kuwa gari aina ya Landcruiser VX iligonga daladala hiyo iliyo kuwa imesimama kupakia abiria kwenye kituo kimoja maarufu kwa jina la Kona. Ajali hiyo imetokea muda wa saa 10.30 jana jioni.
Gari aina ya Landcruiser VX iliyokuwa na wanafunzi toka chuo cha Mweka ikiwa imezama kwenye mtaro na kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo mbaya iliyotokea jana jioni.
Pichani ni mashuhuda walikokuwa eneo la tukio wakilitazama gari aina ya landcuriser iliyokuwa imezama kwenye mtaro baada ya ajali hiyo iliyotokea na kusababisha majeruhi.
Daladala iliyogongwa vibaya na Landcuriser ikiwa imeharibika vibaya ubavuni kiasi cha kutoweza kutembea tena lakini Taarifa za awali hali ya dereva wake inasemekana kuwa mbaya pia idadi ya majeruhi mpaka tunaenda mitamboni haijajulikana.tutaendelea kukujuza jinsi taarifa zitakavyofikia kuhusu hali na idadi Ya majeruhi.PICHA NA HABARI NA mdau WITO MSAFIRI WA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG