Akizungumza kwenye kikao hicho Mkuu wa polisi wilaya ya Makete (OCD) Alfred Kasonde amekanusha vikali tuhuma zinazoelekezwa kwa askari wake kuwa wanakula fedha wanazotoza kama faini kwa vyombo vya usafiri wanavyotoza kutokana na makosa mbalimbali na kuongeza kuwa ni vingumu kwa askari ambaye amekuandikia faini ya kosa lako kwenye kitabu cha serikali kula fedha hiyo
Bw. Kasonde amesema askari wake hawana vitabu vya risiti na hawaruhusiwi kutembea navyo kwa kuwa jeshi la polisi lina wahasibu wanaokusanya fedha hizo, hivyo kwa wilaya ya Makete dereva akiandikiwa faini na askari, askari haruhusiwi kupokea fedha na badala yake atakuandikia karatasi maalum maarufu kama notification na baada ya hapo dereva huyo atakwenda kulipa faini hiyo kituoni
Amewataka madereva hao kuacha kuwapa fedha ya faini askari hao na badala yake wahakikishe askari aliyewakamata anaandika kosa hilo kwenye kitabu cha faini, huku akionesha rundo la risiti za madereva bodaboda ambao wamelipia faini lakini hawajafika kuchukua risiti zao kwa madai kuwa fedha walizotoa zililiwa na askari
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Makete mh. Josephine Matiro amewataka madereva hao kuhakikisha wanajikamilisha kwa vitu vyote vinavyohitajika kama sheria za usalama barabarani zinavyolelekeza ili kuepukana na adha ya kukamatwa mara kwa mara na askari na kutozwa faini
Mh Mariro amesema ni kweli madereva wengi hawajui sheria za usalama barabarani lakini sheria hazitambui kuwa hawafahamu sheria, hivyo ili kuepukana na adha hiyo wanatakiwa kuwa na vitu vyote vinavyohitajika kama leseni ya udereva, leseni ya biashara, bima, kadi ya pikipiki, stika ya nenda kwa usalama, kofia ngumu(helment 2) pamoja na pikipiki yenye vyake vifaa vyote
Amesema kwa kulitambua hilo mkuu huyo atafanya mazungumzo na chuo cha VETA Makete kifanye mafunzo maalum kwa madereva hao kwa gharama nafuu ili wazifahamu sheria za usalama barabarani pamoja na kupata leseni za udereva