Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar yabadilishana majengo na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

$
0
0

01

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Salum Ali wa kwanza (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ wa kwanza (kulia) wakitia saini makubaliano ya ubadilishanaji  majengo ya Taasisi hizo mbili katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya Kiislamu ya PBZ Mpirani mjni Zanzibar. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ Abrahamani Mwinyi.

02

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Salum Ali wa kwanza (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ wa kwanza (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya ubadilishanaji majengo ya Taasisi hizo mbili ambapo PBZ itachukua jingo la Ofisi ya Biashara ya Magari liliopo Malindi na Wizara ya Biashara itachukua Jengo la Makao Makuu ya sasa ya PBZ la Darajani

 03

Baadhi ya Maofisa wa PBZ wakiangalia utiaji saini wa makubaliano ya ubadilishanaji wa majengo ya Benki hiyo na iliyokuwa Ofisi ya Shirika la Biashara ya Magari lililochini ya Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.

 04

 Picha ya pamoja ya maafisa wa PBZ na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko baada ya kumalizika hafla ya makubaliano ya ubadilishanaji wa majengo ya Taasisi hzo mbili iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya kiislamu ya PBZ Mpirani mjini Zanzibar.

05

Jengo la Ofisi ya Biashara ya Magari liliopo Malindi Mjini Zanzibar ambalo limekabidhiwa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa ajili ya kujenga Makao Makuu Mapya ya Benki hiyo.

06

Jengo la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) liliopo Darajani Mjini Zanzibar ambalo limekabidhiwa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles