Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Kanisa la Mtakatifu Peter Oysterbay, leo asubuhi kwa ajili ya kushiriki katika Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa hilo. ambapo zaidi ya Sh. milioni 65 zilipatikana kati ya Sh. milioni 600, zinazohitajika hadi ifikapo mwezi Julai. Kati ya hizo Cash ni Sh. milioni 5 na zilizobakia zikiwa ni ahadi.(Picha na OMR).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais Mtaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, wakishiriki katika Misa maalum ya Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Jan 26, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kikristu wakati wa Ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Jan 26, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwadhama Cardinali Polycap Pengo, wakati wa ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akisalimiana na Mwadhama Cardinari Polycap Pengo, wakati wa ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.