Msemaji wa Kamati ya Kuratibu Mazishi ya Msanii Albert Mangwea aliyefariki nchini Afrika Kusini akiwa katika shughuli zake za kimuziki Adamu Juma (kushoto) akitoa taarifakwa vyombo vya habari kuwa kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa mwili wa mwanamuziki huyo unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumamosi Jioni.
Aidha amesema mwili huo unatarajiwa kuagwa siku ya Jumapili saa 2 asubuhi kabla ya kusafirishwa kuelekea Mororgoro Kihonda kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika tarehe 3 Mwezi wa Sita mwaka huu.
Adamu Juma ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kujitolea michango ili kufanikisha msiba huo.
Unaweza kutuma mchango wako kwenye Namba ya Kaka wa marehemu Keneth Mangwea +255-754-967738 ambayo imeunganishwa na M-Pesa ili kufanikisha za mazishi ya mpendwa wetu.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.