Msemaji wa Smile Communications Tanzania Santina Benson akitambulisha meza kuu ya wasemaji wa kampuni hiyo katika kikao cha waandishi wa habari ambapo leo wametangaza rasmi kwa Umma wa Watanzania wamezindua Mtandao wa Intaneti wa 4G LTE ambayo ni ya kwanza na ya kipekee nchini Tanzania.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Smile Group, Irene Charnely akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana uzinduzi rasmi biashara yao ya intaneti inayoongoza nchini Tanzania ya Fourth Generation Long Term Evolution (4G LTE) na kuongeza kuwa Smile ilianza mapinduzi katika nyanja ya mawasiliano Afrika Mashariki ndipo ilipoichagua Tanzania kama nchi ya kwanza katika kuanzisha mtandao wake wa intaneti ya 4G LTE. Kushoto ni Meneja Mkazi wa Smile Tanzania Fiona McGloin.
Head of Network Planning wa Kampuni ya Smile Communication Tanzania Ltd. Madaha Francis akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ambapo amesema kwa mwaka huu mtandao 4G LTE unashika sehemu kubwa ya Dar es Salaam na kuahidi kuwa mwisho wa mwaka kesho watakuwa wameifikia mikoa mikubwa mitano ya Tanzania na ndani ya miaka 5 ijayo watakuwa wameifikia mikoa yote ya nchini
Bw. Madaha ameongeza kuwa katika kurudisha fadhila kwa jamii kampuni yake imeunganisha shule 10 za Dar es Salaam na mtandao wa wa 4G LTE na kuwapa 20 GB za bure kila mwezi kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi zaidi wa masuala ya ICT ukizingatia Teknolojia inakuwa kwa kasi zaidi dunia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Smile Group, Irene Charnely akijibu maswali kwa waandishi wa habari ambapo ameishukuru na kuipongeza TCRA pamoja na Serikali ya Tanzania kwa kutoa fursa nzuri iliyowazi kwa wawekezaji wa nje kuwekeza nchini. Kulia ni Head of Network Planning wa Kampuni ya Smile Communication Tanzania Ltd. Madaha Francis na kushoto ni Meneja Mkazi wa Smile Communication Tanzania Fiona McGloin.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakijionea kwa macho yao kasi ya ajabu ya Mtandao wa Intaneti wa 4G LTE uliotambulishwa rasmi leo na kuwapa mwanya Watanzania kwa Ujumla kuutumia bila kwikwi kama mitandao mingine iliyotangulia nchini.
Baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali za kampuni ya Smile Communication Tanzania.
Smile Communications Tanzania (“Smile TZ”), ni sehemu ya Smile Telecoms Holdings Limited (“Smile”) (ikiwa inafahamika zaidi kama Smile), leo inazindua rasmi biashara yake ya intaneti inayoongoza nchini Tanzania ya Fourth Generation Long Term Evolution (4G LTE)
Mnamo 2012, Smile ilianza mapinduzi katika nyanja ya mawasiliano Afrika Mashariki ilipoichagua Tanzania kama nchi ya kwanza katika kuanzisha mtandao wake wa intaneti ya 4G LTE. Baada ya muda wa zaidi ya mwaka mmoja wa majaribio endelevu na kupata mchango mathubuti kutoka kwa wadau wa teknolojia na wateja wetu wa majaribio, Smile ilianza kuuza intaneti kwa wateja wake wa sasa ambao wanatofautiana, kuanzia – makampuni madogo mpaka yenye ukubwa wa kati na watumiaji wa nyumbani, pia katika maeneo yenye watumiaji wengi wa Wi-Fi (Hotspot) na kwa wakazi wote wa Dar es salaam. Intaneti ya Smile 4G LTE, sasa inapatikana jijini Da es salaam na wateja wanaweza kulipia ili kupata huduma ya intaneti kutoka Smile.
Mtandao wa intaneti ya Smile 4G LTE unatumia teknolojia ya hali ya juu ya huduma za mawasiliano ikiwa na viwango bora vinavyopatikana sehemu tofauti duniani, na italeta kasi yenye utofauti, uhakika, ubora na urahisi wa kuitumia.
Intaneti ya 4G LTE inatuwezesha kuperuzi kwenye tovuti tofauti kwa kasi zaidi, inaongeza uwezo wa mtandao kupenya na kuboresha kwa kiasi kikubwa matumizi yako ukiwa kwenye mtandao tofauti na awali. Kiwango cha ubora wa intaneti ya Smile 4G LTE ni kiwango bora zaidi cha teknolojia ya mawasiliano ya simu duniani kwa sasa. Misingi thabiti ya mtandao huu na uboreshwaji unaoenda sambamba na maendeleo duniani, unatoa uhakika kwamba utabakia kuwa wa ubora wa juu katika matumizi ya data kwenye simu na huduma za sauti kwa miaka mingi ijayo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Smile Group, Irene Charnely, faida za intaneti ya 4G LTE zinathibitishwa vizuri zaidi na watumiaji wapya waliojionea utofauti, na uwezo wa teknolojia hii ya kimataifa kuimarisha upatitikanaji wa njia za mawasiliano zilizoendelea zaidi huku ukipunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji wa shughuli. “4G LTE inafanya wateja wetu waamini kuwa upatikanaji huduma bora ya intaneti ni jambo linalowezekana kutokana na ubora wa huduma wanayoipata” anasema Charnely. “Kuperuzi intaneti, kupakua muziki na filamu bila tatizo, kuwasiliana kwa njia ya sauti ya HD au kupiga simu kwa njia ya video bila wasiwasi – sasa matumizi ya intaneti yamekuwa bora, ya haraka, rahisi na ya uhakika zaidi.
Fiona McGloin, meneja wa Smile Tanzania , anaona kuanzishwa kwa 4G LTE ni moja ya hatua kubwa katika maendeleo ya Afrika Mashariki na bara la Afrika kwa ujumla. “Kwa uzoefu wetu katika kutoa huduma kwa wateja wetu katika kipindi cha miezi sita iliyopita jijini Dar es salaam, tumefanikiwa kuhakikisha upatikanaji wa intaneti yenye ubora, iliyo rahisi zaidi, ikiwa na teknolojia yenye kasi zaidi sehemu yeyote duniani. Jambo hilo limeleta matokeo ya kuongezeka kwa kiwango cha matumizi na mahitaji ya huduma zetu” anasema.
Kwa mujibu wa Charnley, “Kuanzishwa na upatikanaji wa teknolojia ya intaneti ya 4G LTE kutaleta mabadiliko kwa Watanzania na Tanzania kwa ujumla katika sekta za maendeleo huku kukiongeza matumizi ya mtandao kwa njia ya simu katika bara la Afrika, hivyo kuimalisha shughuli za kiuchumi. Tumekuwa tukisubiri na kutumaini juu ya mabadiliko siku za usoni lakini tukiwa na intaneti ya 4G LTE, mabadiliko chanya ndiyo haya”
Smile Communications mpaka sasa wanatoa huduma katika nchi tano tofauti barani Afrika, ikiapo Tanzania.
“Kampuni ilianzishwa katika mtazamo rahisi tu – kutoa huduma za mawasiliano za bei nafuu, zenye ubora wa juu na kuwa mtandao rahisi kuutumia na kupatikana kwa kila mmoja barani Afrika, ukitumia gharama ndogo na njia za kisasa za biashara pamoja na teknolojia inayoenda na wakati” anasema Charnley. “Leo kampuni hii imeshapiga hatua katika kukamilisha mtazamo huo kuwa kweli”
Mtandao wa intaneti ya Smile 4G LTE ambao sasa unapatikana jijini Dar es salaam, utaendelea kupanuka kuelekea mikoani mingine ya Tanzania kwa awamu tofauti zitakazochukua muda wa miaka miwili.
Wateja wanaotaka kujiunga na kujionea utofauti wa intaneti ya Smile 4G LTE, wanaweza kutembelea maduka ya Smile yaliopo Regent Business Park (Mikocheni), Viva Towers (Upanga) au Shamo Trade Tower & Shopping Center (Mbezi Beach). Sehemu nyingine za mauzo ni vioski cha Smile vilivyopo Shoprite Supermarket (Mlimani City Mall) na TSN Supermarkets (Bamaga, Upanga, Baraka Plaza, Tegeta). Wateja wanaweza kutembelea pia tovuti ya Smile ambayo ni www.smile.co.tz