Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Mhe. Kombani awapongeza wanamichezo OR-MUU kwa ushindi mkubwa

$
0
0

IMG_5882

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Mh. Celina O. Kombani (Mb) akikabidhiwa kombe la ubingwa wa Mpira wa Pete la Mei Mosi 2014 kutoka kwa Kapteni wa timu Elizabeth Fusi katika hafla fupi aliyoiandaa kuwapongeza mabingwa hao mapema leo ukumbi wa Utumishi. (Picha Na. Happiness Shayo).

Na Mary Mwakapenda

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR MUU), Mhe. Celina O. Kombani amesema michezo ni sehemu ya maisha na hujenga afya bora hivyo kuleta tija katika kazi.

Mhe. Kombani alisema hayo katika hafla fupi aliyoiandaa ofisini kwake ili kuwapongeza wachezaji wa Mpira wa Pete wa OR MUU kwa kunyakua Kombe la Mei Mosi 2014 katika mashindano yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Mhe. Waziri aliwadokeza wanamichezo hao, na watumishi wa ofisi yake kuwa michezo hupunguza maradhi hususan  magonjwa yasiyoambukiza na hata yale yanayoambukiza kama vile ugonjwa wa moyo, kisukari na maambukizi ya VVU.

“Michezo hupunguza mawazo na kuleta mahusiano mema kazini” Mhe. Kombani alisema.

Waziri Kombani alisema ushindi wa timu ya Mpira wa Pete umejenga jina la ofisi yake na kuwa mfano wa kuigwa kwa wengine na kuwaasa wanamichezo hao kuendelea na moyo wa kujituma, kuwa na nidhamu ili waweze kutetea ushindi walioupata.

Alisema OR MUU ni kioo hivyo iwe mifano katika michezo na kazi. Aidha aliongeza watumishi wajipange kushiriki katika michezo mingine inayoshindaniwa.

Akitoa salamu za shukrani Naibu Katibu Mkuu, Bw. HAB Mkwizu alisema masuala yote yatafanyiwa kazi na kuwaelekeza viongozi wa michezo kuandaa michezo mara moja kwa kila mwezi (Bonanza) ili kuwakutanisha watumishi na kujenga timu imara za michezo mingine.

Ushindi wa OR MUU ulipatikana baada ya kushinda kwa kishindo michezo yake ya awali na fainali kuilaza Wizara ya Uchukuzi kwa magoli 33 dhidi ya 21. Kombe hilo lilikuwa likishikiliwa na timu ya Wizara ya Ulinzi iliyokuwa bingwa katika mashindano yaliyopita Mwaka 2013.

Mashindano hayo yalianza tarehe 14 Aprili, 2014 na kumalizika tarehe 28 Aprili, 2014 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Latest Images

Trending Articles



Latest Images