Goli la dakika za nyongeza kutoka kwa Branislav Ivanovic limeisaidia Chelsea kuwa klabu ya kwanza ya Uingereza, kushinda mataji yote matatu makubwa ya UEFA, baada ya kuishinda Benfica kwa magoli 2-1 katika fainali za Ligi ya Europa mjini Amsterdam usiku wa kuamkia leo.
Branislav Ivanovic akishangilia baada ya kuitandika bao Benfica.