Quantcast
Channel: MO BLOG » Admin
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Jela miaka nane kwa kosa la kumuua mumewe

$
0
0

Jail-Cell

Na Nathaniel Limu, Singida

MAHAKAMA kuu kanda ya kati inayoendelea na vikao vyake mjini Singida,imemhukumu Magreth Omari Mshanangu (52) mkulima mkazi wa kijiji cha Nguvumali wilaya ya Iramba,adhabu ya kutumikia jela miaka nane baada ya kukiri kosa la kumuuawa mume wake Daudi Mlangi bila kukusudia.

Pia mtoto wa mshitakiwa Magreth,Shaban Hassan @ Benjamini (22),naye amehukumiwa adhabu ya kutumikia jela miaka minane baada ya kukiri kosa la kumuuawa baba yake wa kambo Daudi Mlangi bila kukusudia.

Mshitakiwa Shaban ni mkazi wa kijiji cha Mlandala kata ya Ndago wilaya ya Iramba mkoa wa Singida.

Awali washitakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia,lakini mahakama hiyo ilibadilisha kosa na kuwa la kuuawa bila ya kukusudia.

Mapema mwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Caren Mrango,alidai mbele ya jaji wa mahakama kuu Cresentia Makuru,kuwa mnamo aprili mbili mwaka 2012 saa saba mchana huko katika kijiji cha Nguvumali wilaya ya Iramba,washitakiwa kwa pamoja walimnyonga hadi kufa Daudi Mlangi.

Amesema kuwa wanandoa hao ndoa yao ilikuwa ilikuwa imetawaliwa na misuguano na ugomvi wa mara kwa mara.

Mrango amesema siku ya kutukio,marehemu Mlangi alirejea nyumbani saa saba mchana na baada ya muda mfupi,ugomvi ulizuka baina ya wana ndoa hao na kisha kuanza kupigana.

Amesema katika ugomvi huo,Magreth aliweza kumng’ata kwa meno mume wake katika sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo miguuni.Wakati huo huo Shaban alikuwa akijimnyonga baba yake wa kambo shingoni kwa kutumia kamba.

Mwanasheria huyo amesema katika hekaheka hizo,zilisababisha kukatisha maisha ya Daudi Mlangi.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo,wakili wa kujitegemea Raymond Kimu,aliiomba mahakama hiyo iwaonee huruma wateja wake kwa vile kosa hilo ni la kwanza kwanza kwao toka wazaliwe na kwamba hawajaisumbua mahakama kwa kitendo chao cha kukiri kosa la kuuawa bila kukusudia.

Jaji Makuru amesema kwa kuzingatia maelezo ya pande zote mbili,mahakama hiyo imefikia uamuzi wa kutoa hukumu ya adhabu ya kutumikia jela kila mmoja miaka nane ili iwe fundisho kwao na watu wengine wanaotarajia kutenda kosa la aina hii.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1758

Trending Articles